Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania aitaka Taifa Stars

MTANZANIA Pict

Muktasari:

  • Santos ameongeza anaamini wakipambana na kuonyesha kiwango bora wana nafasi ya kupanda daraja hadi kucheza ligi daraja la tatu msimu uliopita kwani hadi sasa inaongoza kwenye mechi sita ikikusanya pointi 13.

MCHEZAJI wa Kitanzania anayekipiga Ceu Ciutat Meridiana inayoshiriki Ligi Daraja la Nne, Hispania (Catalunya), Fahmar Santos amesema ndoto yake kubwa kwa mwaka huu ni kupata nafasi katika kikosi cha timu ya taifa, licha ya kutambua ushindani wa kufikia hatua hiyo ni mkubwa na unahitaji juhudi zaidi.

Santos amesema anaendelea kupambana katika klabu ili kuimarisha kiwango na kujiongezea nafasi ya kutimiza ndoto hiyo na kucheza timu ya taifa ni moja ya malengo anayoyatamani.

"Asante, acha nipambane mwaka huu. Natamani nije kucheza timu ya taifa, ila ndiyo hivyo, ni ngumu sana lakini naamini kwenye upambanaji nitacheza," amesema Santos.

Akizungumzia mwenendo wake katika kikosi hicho, Santos ameongeza, amekuwa akipata nafasi ya kucheza na hadi sasa akikipiga dakika 360.

Alieleza katika takwimu zake za michezo aliyocheza, kuna mechi alizoanza kikosi cha kwanza, nyingine alikuwa benchi.

"Jambo zuri ni licha ya kuuguza majeraha ndani ya mwaka mzima lakini makocha wananiamini na wanaona uwezo wangu."

Santos ameongeza anaamini wakipambana na kuonyesha kiwango bora wana nafasi ya kupanda daraja hadi kucheza ligi daraja la tatu msimu uliopita kwani hadi sasa inaongoza kwenye mechi sita ikikusanya pointi 13.