Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hawa ndio mastaa mafundi uwanjani

MAFUNDI Pict

Muktasari:

  • Mwanaspoti limepiga stori na baadhi ya makocha na wachezaji wa zamani waliowatajwa baadhi ya wachezaji wenye ufundi na maarifa makubwa wawapo uwanjani, ingawa baadhi yao wanasema inategemeana na mbinu na mipango ya kocha.

KUNA upekee wa kila mchezaji anapokuwa uwanjani, kama ambavyo wanatajwa baadhi kuonekana kuwa na ufundi mwingi unaokuwa faida kwa timu husika.

Mwanaspoti limepiga stori na baadhi ya makocha na wachezaji wa zamani waliowatajwa baadhi ya wachezaji wenye ufundi na maarifa makubwa wawapo uwanjani, ingawa baadhi yao wanasema inategemeana na mbinu na mipango ya kocha.

Kocha wa Mashujaa, Amani Josiah anasema ukiondoa wachezaji waliopo Simba, Yanga na Azam FC timu zenye mastaa wanaocheza kiufundi, kutoka timu zingine baadhi yao ni nahodha wa Namungo, Jacob Masawe na Haruna Chanongo wa Mashujaa.

MAFU 04

“Masawe na Chanongo wakiwepo uwanjani kocha unakuwa hauna maelekezo mengi ya kuwaambia, wakati mwingine wanakuwa kama makocha wasaidizi, wanatumia ufundi mwingi, kitu ambacho wachezaji wengi wanakuwa wanakikosa,” anasema Josiah na kuongeza:

“Hiyo ndiyo sababu ya maswali mengi ya kwa nini wachezaji wazawa wanapojiunga Simba na Yanga wanakuwa wanashindwa kupata nafasi za kucheza vikosi vya kwanza, ukweli wanakuwa hawana levo za viwango vya ufundi na mara nyingi makocha wazungu wanakuwa hawana muda wa kumwelekeza mchezaji, jambo moja kwa muda mrefu, badala yake wanatumia wale wenye utayari ili kuwapa matokeo ya ushindi.”

MAFU 06

Anasema asilimia kubwa ya wachezaji waliopo Simba na Yanga, wanacheza kwa ufundi zaidi:”Ndiyo maana Simba na Yanga zinapokutana na timu za madaraja ya kati, tunakuwa tunacheza nazo kwa akili kubwa ili kuweza kumenteini mchezo.”

Kocha Mecky Maxime anamtolea mfano Masawe kuwa anayejitoa sehemu kubwa ya uwanja, anatambua majukumu yake ya kipi akifanye kwa wakati gani  “Ukimuweka Masawe kwenye ubora wa kiuchezaji ni mkubwa na nidhamu yake ipo juu. Hao ni miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa kwenye timu na makocha siyo rahisi kuwaacha,” anasema Maxime.

MAFU 03

Mussa Hassan Mgosi, kocha wa Simba Queens, anasema ili kumtambua mchezaji anayetumia ufundi zaidi uwanjani, jambo la kwanza ni watu wanaomzunguka.

“Mfano kipindi nilichokuwa nacheza na kocha wa Simba alikuwa Patrick Phiri alikuwa ananiambia, uchambuzi wako wa masuala ya soka tunapojadili kuhusu timu ni wa kiufundi, unavyofanya mazoezi una-tumia ufundi asilimia 80 na 20 ni kipaji chako na alinitabiria nitakuwa kocha,” anasema Mgosi na kuongeza:

MAFU 02

“Kinachotakiwa kwa asilimia kubwa, mchezaji anapaswa kucheza kwa ufundi asilimia 70 hadi 80, zinazobakia inakuwa kipaji chake, ingawa kuna wakati kulingana na mechi kocha anaweza akamwambia mchezaji wewe kavuruge eneo fulani ili kuwaondolea wapinzani fokasi, hivyo usiende kutumia ufundi, ndiyo maana nimesema watu wanaomzunguka ni rahisi kuujua ufundi wake.”

Anasema asilimia kubwa ya wachezaji wanaokuwa na ufundi mwingi ni magolikipa, mabeki ambao wanauona mchezo kwa ukubwa, ndiyo maana wanapaswa kushauriana na wenzao ili kujua kipi wakifanye, wengine wanaoingia hapo ni viungo.

Staa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Sekilojo Chambua kuhusu Chanongo anasema ni mchezaji aliyekuwa amempandisha kutoka kikosi B cha Polisi Dodoma msimu wa 2008/9, aliona kipaji chake akampeleka katika kikosi cha Wanajangwani, baada ya kuona hana nafasi akaona bora aende Simba.

MAFU 05

“Ukiachana na hao wachezaji waliotajwa na makocha wengine, mimi nitachanganya wazawa na wageni, mfano wapo kama kina Idd Nado, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kutoka Azam kwa wageni ni kama Maxi Nzengeli, Aziz Ki, Elie Mpanzu, Libasse Guèye na Clatous Chama, wana muendelezo wa kiwango,” anasema Chambua na kuongeza:

“Japokuwa Chama kutokana na umri wake kwenda anacheza taratibu, Aziz Ki pia anacheza taratibu lakini ni miongoni mwa watu wenye maarifa makubwa ya mpira wa miguu.”


MAFU 01

KAULI ZA WACHEZAJI

Anasema nafasi anayocheza na umbile lake vimechangia kucheza kwa ufundi, ingawa anasisitiza kila mchezaji ana kitu chake cha kipekee ambacho mwingine anakuwa hana.

“Kitu kinachonipa moyo na kuendelea kujifunza zaidi ni makocha ambao wamewahi kuniambia moja kwa moja ukiacha kocha Josiah kumsikia katika mahojiano yake, makocha wengine waliowahi kunieleza hilo ni Maxime, Cedric Kaze, Patrick Liewig, Kitambi na Emmanuel Masawe,” anasema.

Kwa upande wa Chanongo anasema: “Jicho la kocha linaona zaidi, hivyo nashukuru kama anaona ni miongoni mwa wachezaji wanaofanya kazi nzuri.”

Ukiachana na mastaa wa sasa, aliyekuwa kiungo wa wa Yanga na Simba, Haruna Niyonzima aliwahi kusema: “Miongoni mwa mafundi niliyowahi kuwashuhudia Tanzania ni Shaban Kisiga, jamaa anajua mpira na maarifa yake ni makubwa.”