Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi aita sura mpya Taifa Stars 

Muktasari:

  • Kikosi hicho kilichotangazwa leo Jumamosi, Oktoba 31, 2026 ni kwa ajili ya mechi mbili za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 dhidi ya Nigeria zitakazochezwa Novemba 13 na Novemba 17 mwaka huu.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi amewaweka kando idadi kubwa ya wachezaji waliokuwepo katika  kikosi cha timu hiyo kilichocheza dhidi ya Guinea Bissau na Madagascar mwezi Septemba.

Kikosi hicho kilichotangazwa leo Jumamosi, Oktoba 31, 2026 ni kwa ajili ya mechi mbili za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 dhidi ya Nigeria zitakazochezwa Novemba 13 na Novemba 17 mwaka huu.

Miongoni mwa nyota ambao wameenguliwa kikosini ni Tarryn Allarakhia, Yusuph Kagoma, Mudathir Yahya, Mohamed Hussein, Yona Amos, Metacha Mnata, Pascal Msindo na Hussein Masalanga.

Baada ya kukaa muda mrefu nje ya kikosi, kiungo mshambuliaji Ben Starkie anayeichezea Truro City ya England amerudishwa tena kikosini kama ilivyo kwa  Clement Mzize.

Kwa mara ya kwanza, Gamondi amemjumuisha kikosini beki wa kati wa Kagera Sugar, Evastus Lukanima aliyeonyesha kiwango bora akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya Umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’.

Sura mpya nyingine katika kikosi cha Taifa Stars ni kipa Abdallah Hamisi anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Al Ain inayoshiriki Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu.

Nyota wawili wa Yanga waliokuwa majeruhi kwa muda mrefu, Dickson Job na Clement Mzize nao wamejumuishwa katika kikosi hicho cha Taifa Stars.

Wachezaji 24 wametangazwa kuunda kikosi hicho chenye mchanganyiko wa wachezaji wanaocheza soka ndani na nje ya nchi.

Kikosi kinawajumuisha makipa Aishi Manula, Zuberi Foba na Abdallah Hamisi.

Mabeki ni Evastus Lukanima , Ibrahim Abdullah, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Haji Mnoga, Anthony Mligo na Nathaniel Chilambo.

Viungo ni Alphonce Mabula, Himid Mao, Novatus Miroshi, Ben Starkie, Feisal Salum  na Sheikhan Khamis.

Washambuliaji ni Abdul Sopu, Simon Msuva, Kibu Denis, Charles M’Mombwa, Cyprian Kachwele, Seleman Mwalimu, Clement Mzize na Bernard Kamungo.