Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Milioni 50 za Mixx zampa Mohammed tumaini jipya

MBIO Pict

Muktasari:

  • Mohammed ndiye mshindi wa zawadi kubwa zaidi katika kampeni hiyo iliyoendeshwa na Mixx kwa ushirikiano na Hisense kwa kipindi cha takribani miezi miwili, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Kombe la Dunia sambamba na kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali.

USHINDI wa Sh50 milioni kupitia kampeni ya 'Kila Muamala ni Bao la Ushindi' umegeuza ndoto ya mkazi wa Vikindu, Mohammed Misanga, kuwa karibu na uhalisia baada ya kutangaza kuwa sehemu ya fedha hizo atazitumia kujenga kituo cha afya kitakachohudumia wananchi wa eneo lake.

Mohammed ndiye mshindi wa zawadi kubwa zaidi katika kampeni hiyo iliyoendeshwa na Mixx kwa ushirikiano na Hisense kwa kipindi cha takribani miezi miwili, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Kombe la Dunia sambamba na kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali.

Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Angelica Pesha, alisema kampeni hiyo imekuwa zaidi ya promosheni ya zawadi kwani imekuwa daraja la kutimiza ndoto za Watanzania wengi.

"Hii imekuwa zaidi ya kampeni. Tumeona ndoto za wateja wetu zikitimizwa. Kila mshindi ameeleza namna ushindi wake ulivyobadilisha maisha yake, wengine wameongeza mitaji, wamelipa ada, wamesafiri nje ya nchi kwa mara ya kwanza na wengine wamejikwamua kiuchumi. Hiyo ndiyo maana halisi ya kauli mbiu yetu ya Kila Muamala ni Bao la Ushindi," alisema Pesha.

Alisema kampeni hiyo imeongeza matumizi ya huduma za Mixx huku maelfu ya miamala ikifanyika kupitia huduma mbalimbali ikiwemo kutuma na kupokea fedha, kulipa bili, kufanya malipo kwa wafanyabiashara kupitia Lipa kwa Simu, kuwekeza pamoja na kutumia Mixx Super App.

Pesha aliongeza kuwa Mixx itaendelea kubuni huduma zitakazorahisisha maisha ya Watanzania huku akiishukuru Hisense, vyombo vya habari, watayarishaji wa maudhui na wateja kwa kufanikisha kampeni hiyo.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Mars Communications anayewakilisha Hisense, Tahera Karim, alisema ushirikiano huo umeonyesha namna sekta binafsi zinavyoweza kushirikiana na kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa jamii.

"Tulianza kampeni hii tukiwa na lengo la kuwazawadia wateja wetu, lakini leo tunaona zawadi hizo zimekuwa chanzo cha matumaini kwa jamii. Ndoto ya Mohammed ya kujenga kituo cha afya inaonyesha kuwa ushirikiano wetu na Mixx umevuka mipaka ya biashara na kugusa maisha ya watu," alisema Karim.

Mshindi huyo, Mohammed Misanga, alisema hadi siku moja kabla ya kukabidhiwa zawadi alikuwa bado haamini kama kweli ndiye mshindi wa Sh50 milioni.

Alisema pamoja na kuwasaidia wazazi wake, kipaumbele chake ni kutekeleza ndoto aliyokuwa nayo kwa muda mrefu ya kuanzisha kituo cha afya kitakachowahudumia wakazi wa Vikindu na maeneo ya jirani.

"Nawashukuru sana Mixx na Hisense kwa kampeni hii iliyobadilisha maisha yangu. Kupitia ushindi huu sasa nina nafasi ya kutimiza ndoto yangu ya kujenga kituo cha afya kitakachoboresha huduma za afya kwa wakazi wa Vikindu na maeneo yanayozunguka," alisema Mohammed.

Zaidi ya Watanzania 100 walinufaika na kampeni hiyo kwa kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, vifaa vya kielektroniki vya Hisense pamoja na safari ya kwenda Mexico kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia.