Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgunda: Timu haijengwi kwa siku moja jamani

MGUNDA Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti Mgunda amesema mpira wa miguu ni mchakato unaohitaji hatua kwa hatua, hasa kwa timu inayofanya mabadiliko ya kikosi na kuingiza wachezaji wapya ambao wanahitaji muda wa kufahamiana, kuelewa mfumo wa kocha na kujenga maelewano uwanjani.

KOCHA wa Namungo, Juma Mgunda, amesema ujenzi wa kikosi kipya unahitaji muda na subira, akieleza kuwa hawezi kutarajia timu yake kufikia kiwango kinachotakiwa ndani ya muda mfupi wakati haikupata maandalizi ya kutosha kabla ya kuanza kwa msimu.

Akizungumza na Mwanaspoti Mgunda amesema mpira wa miguu ni mchakato unaohitaji hatua kwa hatua, hasa kwa timu inayofanya mabadiliko ya kikosi na kuingiza wachezaji wapya ambao wanahitaji muda wa kufahamiana, kuelewa mfumo wa kocha na kujenga maelewano uwanjani.

Kocha huyo amesema changamoto hiyo imeongezwa na ratiba ya msimu huu, ambapo ligi iliyopita ilichelewa kumalizika wakati msimu mpya ukaanza mapema, hali iliyozifanya timu nyingi kukosa muda mzuri wa kufanya maandalizi ya msimu.

MGU 08

“Unapotengeneza timu mpya unahitaji muda na subira, kwa sababu mpira ni process, siyo kama unaweka chumvi kwenye mboga halafu ikakolea mara moja. Ni mchakato wa hatua kwa hatua,” amesema Mgunda.

Amesema hali hiyo imeifanya timu yake kutumia kipindi hiki cha mapumziko kama nafasi ya kuongeza muda wa mazoezi na kurekebisha mapungufu yaliyoonekana katika michezo ya mwanzo wa msimu.

“Kwa sababu tulikosa muda wa pre-season, hizi wiki tatu tunazitumia kama semi pre-season. Tunataka kutumia muda huu kurekebisha mapungufu na makosa yetu yote,” amesema Mgunda.

MGU 09

Kwa Namungo, wiki tatu zilizopatikana za mazoezi zinatumika kama aina ya maandalizi ya katikati ya msimu, au semi pre-season, ambapo benchi la ufundi linapata muda wa kuifanyia kazi timu kwa utulivu zaidi.

Mgunda amekuwa na mwanzo wenye changamoto kwenye msimu huu akiwa ameiongoza Namungo katika mechi saba za ligi, akishinda mbili na kupoteza tano, huku timu ikiwa na pointi sita na kukaa katika nafasi ya 13.