Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgosi aanda dozi Simba Queens

MGOSI (1)

Muktasari:

  • Rekodi hiyo inaifanya timu hiyo kufikisha mwaka mmoja na siku tisa tangu ilipoanza safari yake ya kutopoteza mechi, Novemba 14, 2025, ilipoanza kampeni za msimu wa 2025/26 kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Bilo FC.

KOCHA mkuu wa Simba Queens, Mussa Hassan ‘Mgosi’ amesema atatumia kipindi cha mapumziko ya ligi kuboresha eneo la umaliziaji kwa kuwafanya washambuliaji wake kuongeza umakini katika kutumia nafasi za kufunga.

Mgosi amesema licha ya timu yake kuonyesha ushindani na kupata matokeo mazuri katika michezo yote minne ya mwanzo wa msimu, bado kuna mapungufu yanayohitaji kurekebishwa, hasa katika kutumia nafasi za kufunga zinazotengenezwa na wachezaji wake.

"Tunaenda mapumzikoni na tutatumia muda huo kufanya mazoezi na kurekebisha maeneo ambayo tumeona tuna mapungufu, hasa katika umaliziaji wa nafasi," amesema kocha huyo.

Simba Queens imeanza msimu wa 2026/27 kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kilimanjaro Wonders, bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate Princess na mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa Queens, kabla ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Ceasiaa Queens katika mchezo wa Novemba 18.

Matokeo hayo yanaifanya Simba Queens kuwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi nne, ikiwa imeshinda tatu na kutoka sare moja. Katika michezo hiyo, imefunga mabao sita bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa, takwimu zinazoonyesha uimara wa safu yake ya ulinzi tangu mwanzo wa msimu.

Pamoja na changamoto ya umaliziaji wa nafasi, Simba Queens imeendelea kudumisha rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi, ikiwa imefikisha mechi 26 mfululizo bila kuonja ladha ya kipigo.

Rekodi hiyo inaifanya timu hiyo kufikisha mwaka mmoja na siku tisa tangu ilipoanza safari yake ya kutopoteza mechi, Novemba 14, 2025, ilipoanza kampeni za msimu wa 2025/26 kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Bilo FC.