Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mganga aibuka na Tenga Uwanjani

Muktasari:

MICHUANO ya Sports Xtra Ndondo Cup inayodhaminiwa na Gazeti la Mwanaspoti inazidi kushika kasi na kujaa vituko ambavyo huwezi kuvipata na kuviona kirahisi katika kiwanja chochote kinachotumika na mechi za Ligi Kuu.

MICHUANO ya Sports Xtra Ndondo Cup inayodhaminiwa na Gazeti la Mwanaspoti inazidi kushika kasi na kujaa vituko ambavyo huwezi kuvipata na kuviona kirahisi katika kiwanja chochote kinachotumika na mechi za Ligi Kuu.

Katika mechi iliyopigwa Jumatatu iliyozikutanisha Makumba FC dhidi ya Aggrey mashabiki wa Makumba waliokuwa na kigoma chao walichokuwa wakikipiga huku wadada ambao ni wa timu hiyo walikaa pembeni ila ghafla walilipuka na kuanza kukata mauno huku wakiwa wamevalia madera tu na kuwaacha hoi mashabiki waliokuwa uwanjani hapo wakifuatilia mtanange huo.

Achana na hiyo kiboko ilikuwa juzi usipime katika mechi ya Mtoni City dhidi ya Goms United kama unakua na moyo mdogo unaweza ukatimua mbio.

Lakini usiogope, huwezi kukimbia kutokana na burudani ambazo zinaendelea uwanjani hapo, kama kawaida Mwanaspoti linakuletea mambo yaliyokuwa yanaendelea uwanjani hapo.

 

Mganga aja na tenga uwanjani

Yule Chifu wa FC Kauzu yeye si huwa anakuja na ungo uwanjani!

Sasa mganga wa Mtoni City yeye alitoa kali baada ya kuja katika tenga, huku tenga hilo likiwa limewekwa katika kiti cha nyuma ya baiskeli.

Mashabiki walikuwa wakijiuliza ni kitu gani kinaendelea lakini ghafla aliibuka mganga huyo huku akiwa na kibuyu chake na kufanya mbwembwe zake za kuwavuruga mashabiki wa Goms United kisaikolojia.

 

Mvua ya mawe yaibuka

Kikundi cha ushangiliaji (Masela wa Goms) ambacho kilichelewa kuingia uwanjani hapo kwa kusadikika kuwa kilikuja uwanjani hapo kwa miguu kutoka Gongo la Mboto mpaka Tandika katika Uwanja wa Bandari kilizua kizaazaa.

Masela hao walipofika uwanjani walikuwa wakishangilia kwa kuzunguka uwanja mzima, huku wakiimba nyimbo za kuidifu timu yao ambayo ilikuwa inaongoza bao moja.

Baada ya muda si walijikuta wakianza kurushiana mawe na masela wa Mtoni City ambao walikuwa wametulia baada ya masela wa Goms kuwazomea, walianza kurushiana mawe na baadae polisi waliingilia ugomvi huo na kuwatenganisha mashabiki hao kila mmoja upande wake.

 

Polisi watungiwa nyimbo uwanjani

Baada ya tukio la kurushiana mawe kumalizika mashabiki hao wa Goms waliamua kushangili kwa kuimba: “Tulijua kombati kumbe kaki nguo ya shule, tulijua kombati kumbe kaki nguo ya shule,”walisikika mashabiki hao wakiimba huku wakicheza huku na kule kuwaimbia polisi.

Mashabiki hao pia waliibadili nyimbo ya dini inayoimbwa “Yesu ni wangu wa uzima na milele” na kuwa “Goms ni yangu ya uzima na milele” huku watazamaji wengine wakibaki kuangua vicheko tu kutokana na visanga hivyo vya mashabiki hao wa Goms.

 

Isihaka azinguliwa abadilishe jezi

Beki Hassan Isihaka wa Simba ambaye anaichezea timu ya Goms United inayovaa jezi ya rangi ya njano aliambiwa na mashabiki avue jezi hiyo kwani sio jezi ya chama lake.

“Oya wewe vua ilo lijezi weweeee ilo sio chama lako wala nini wewe yako nyekundu bhana,” alisikika shabiki mmoja huku mashabiki wengine wa Simba wakionesha kuchukizwa na rangi hiyo.

Lakini Isihaka alipoulizwa na mwandishi wa Mwanaspoti alisema rangi hiyo katika Ndondo haimdhuru lakini pia ndio jezi ya timu yake ya kitaani na ndio anaichezea kwahiyo lazima avae tu hana jinsi.

 

Morad ataniwa

Beki aliyemaliza mkataba wake na Azam alijikuta katika wakati mgumu baada ya shabiki mmoja kumzingua kuwa rasta gani anakula nyama huku yeye mwenyewe akiisikia kauli hiyo na aliishia kumuangalia shabiki huyo na kuendelea na soka.

 

Mechi zinazochezwa leo

Mlalakuwa Rangers v Burudani FC (Bandari) na Ndanda v Kibada One (Air Wing) mechi hizo zitaanza saa 10:00, alasiri.