Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfaransa aivaa Singida Black Stars

MFARANSA Pict

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo itakayopigwa keshokutwa Jumapili saa 1:00 usiku, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini, Dar es Salaam, Tusker inaingia ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0, lililofungwa na Mkongomani Jeancy Mboma Kinda dakika ya 52.

KIKOSI cha Tusker FC ya Kenya kimetua Tanzania jana kwa ajili ya mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Singida Black Stars, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Mfaransa Julien Mette akichimba mkwara.

Katika mechi hiyo itakayopigwa keshokutwa Jumapili saa 1:00 usiku, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini, Dar es Salaam, Tusker inaingia ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0, lililofungwa na Mkongomani Jeancy Mboma Kinda dakika ya 52.

Akizungumzia mechi hiyo, Julien amesema licha ya kupoteza nyumbani Kenya ila hawajaja kinyonge Tanzania, huku akiamini wapinzani wao watacheza kwa kutengeneza mashambulizi tofauti na walivyocheza ugenini, walivyotumia mbinu za kujilinda.

“Sisi tulikuwa bora lakini tulipoteza, wapinzani wetu walitumia mbinu za kujilinda na kutunyima nafasi ya kuwashambulia, mechi ya marudiano itakuwa ni ngumu ila, tunatakiwa kutengeneza zaidi mashambulizi ya moja kwa moja, tunaamini kuwa tutaibuka na ushindi na kufuzu hatua inayofuata,” amesema Julien.

Julien amesema kufungwa bao 1-0, hakujakatisha matumaini yao ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe ya Shirikisho Barani Afrika tofauti na ingekuwa mabao 2-0, hivyo, mechi haijaisha na wamefanyia kazi safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho.

Mfaransa huyo amesema miongoni mwa mambo yaliyowagharimu mechi ya kwanza ni kushindwa kutumia vizuri nafasi walizopata za kufunga, jambo ambalo amelifanyia kazi, kwa sababu wana wachezaji wazuri na wenye uwezo wa kutawala mpira uwanjani.