Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi aanika mipango mipya Mtibwa Sugar

ABUSHEHE Pict

Muktasari:

  • Abushehe amejiunga na Mtibwa Sugar ya Morogoro inayopambana kurejea Ligi Kuu Bara, baada ya kushuka msimu wa 2025-2026, ilipomaliza nafasi ya 15 na pointi 27, ikiungana na KMC FC ya Dar es Salaam iliyomaliza nafasi ya 16 na pointi tisa tu.

KIUNGO mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Issa Abushehe 'Messi', amesema licha ya ugeni wake katika timu hiyo msimu huu, ila ataendelea kuonyesha kiwango chake bora, kwa lengo la kukipambania kikosi hicho ili kiweze kurejea tena Ligi Kuu Bara.

Nyota huyo aliyejiunga na Mtibwa Sugar msimu huu akitokea Polisi Tanzania, amesema mechi za raundi ya kwanza ni ngumu kutokana na mahitaji ya kila timu, ingawa yupo tayari kukipambania kikosi hicho kwa kushirikiana na wachezaji wenzake.

"Nashukuru kwa nafasi nyingine niliyoipata hapa Mtibwa Sugar, nimesaidia kuipandisha Polisi Tanzania Ligi Kuu Bara na sasa nataka niendeleze tena rekodi yangu nzuri, siyo rahisi ila naamini kwa umoja wetu tutafanikiwa," amesema Abushehe.

Nyota huyo alijiunga na Polisi baada ya kuachana na Namungo aliyojiunga nayo dirisha dogo la Januari 2025, ikiwa ni muda mfupi tangu avunje mkataba wake wa miezi sita na KVZ, inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar kwa makubaliano ya pande mbili.

Kiungo huyo alijiunga na KVZ kwa msimu wa 2024-2025, akitokea Biashara United ya mkoani Mara iliyokuwa inashiriki Ligi ya Championship, huku akiwahi pia kuzichezea timu mbalimbali zikiwemo za Coastal Union na Al Mokawloon Al Arab ya Misri.

Abushehe amejiunga na Mtibwa Sugar ya Morogoro inayopambana kurejea Ligi Kuu Bara, baada ya kushuka msimu wa 2025-2026, ilipomaliza nafasi ya 15 na pointi 27, ikiungana na KMC FC ya Dar es Salaam iliyomaliza nafasi ya 16 na pointi tisa tu.