Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeya City yatoa siku sita za mapumziko

Muktasari:

  • Mbeya City ilicheza mechi tatu ugenini, ikishinda moja dhidi ya Fountain Gate kwa mabao 2-0, imetoka sare ya bila kufungana na TRA United kabla ya kupoteza 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania. Matokeo hayo yameifanya ikalie nafasi ya sita ikiwa na pointi 10.

BAADA ya kuvuna pointi nne kati ya tisa katika mechi tatu za ugenini, Mbeya City imesema matokeo hayo hayajakidhi matarajio yake katika mpango wa kusaka nafasi nne za juu, huku ikiwa imetoa mapumziko ya siku sita kwa wachezaji wake.

Mbeya City ilicheza mechi tatu ugenini, ikishinda moja dhidi ya Fountain Gate kwa mabao 2-0, imetoka sare ya bila kufungana na TRA United kabla ya kupoteza 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania. Matokeo hayo yameifanya ikalie nafasi ya sita ikiwa na pointi 10.

Baada ya dakika 270 za mechi za ugenini, Mbeya City sasa inatarajia kurejea uwanjani Oktoba 9, 2026 kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa raundi ya saba utakaopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Ofisa Habari wa Mbeya City, Gwamaka Mwankota, alisema kipindi hiki cha mapumziko kupisha kalenda ya FIFA kimetumiwa kuwapa wachezaji nafasi ya kupumzika kwa siku sita kabla ya kurejea kambini kuendelea na mazoezi.

Mwankota alisema pointi nne walizovuna ugenini si matokeo mabaya, ingawa mipango yao ilikuwa kukusanya pointi zote tisa.

“Tulihitaji pointi tisa kwenye mechi tatu za ugenini kwa sababu uwezo tulikuwa nao, lakini tunashukuru kwa kile tulichopata. Tunarejea nyumbani kumsubiri yeyote kuchukua pointi tatu,” alisema.

Alisema mapumziko hayo hayamaanishi kuwa timu imepunguza kasi katika kutimiza malengo yake ya msimu.

“Kwa sababu ratiba imesimama kwa muda, tumewaruhusu wachezaji wapumzike siku sita, kisha warejee kambini kuendelea na mazoezi. Tunayo malengo makubwa sana msimu huu, ndiyo maana hatuna muda wa kupoteza,” alisema Mwankota.

Mbeya City, ambayo msimu uliopita ilinusurika kushuka daraja kupitia mechi za mchujo (play-off), ilianza msimu huu kwa kupoteza dhidi ya Geita Gold, kabla ya kushinda mechi tatu mfululizo, kisha kutoka sare na kupoteza mchezo mwingine.