Kipa Ahmed Issa atoa ahadi kwa, ashabiki wa Coastal Union
Muktasari:
- Alisema, mechi mbili alizopata nafasi ya kudaka dhidi ya Polisi Tanzania na JKT Tanzania, zinatoa muelekeo mzuri upande wake, hivyo hakuna ambacho kitamzuia asitimize malengo yake.
KIPA wa Coastal Union, Ahmed Issa, amewataka mashabiki wa timu hiyo kutegemea mazuri kutoka kwake baada ya kuionja ladha ya Ligi Kuu Zanzibar.
Alisema, mechi mbili alizopata nafasi ya kudaka dhidi ya Polisi Tanzania na JKT Tanzania, zinatoa muelekeo mzuri upande wake, hivyo hakuna ambacho kitamzuia asitimize malengo yake.
“Mechi ya JKT ilikuwa bora sana kwangu hususani kupata nafasi kikosi cha kwanza, naamini nimeonesha kitu ndio sababu kocha akaniamini,” alisema.
Kipa huyo alisema licha ya kuwa hiyo ndio nafasi yake ya kwanza kuichezea Ligi Kuu Tanzania Bara, ameona utofauti mkubwa namna wachezaji wanavyopambania namba kikosini.
Ahmed aliyetua Coastal Union msimu huu akitokea JKU ya Zanzibar, alisema kwa sasa mipango yote ni kufanya vizuri kwa mechi zilizosalia, huku akibainisha kwamba, amefurahi baada ya wachezaji na mashabiki kumsifia kuwa ameanza kwa kufanya vizuri jambo linalompa matumaini.