Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Simba wapewa wiki moja

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho zimeeleza kuwa, kambi imevunjwa kwa muda wa wiki moja, hivyo wachezaji wamepewa nafasi ya kwenda majumbani kwao kwa ajili ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.

MASTAA wa Simba wamepewa wiki moja ya mapumziko baada ya kuvuka kwenye ratiba nzito ya mechi, huku kocha wa kikosi hicho, Steve Barker na wachezaji tayari wamerejea makwao kwa ajili ya kupata muda wa kupumzika kabla ya kurejea tena kambini.

Taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho zimeeleza kuwa, kambi imevunjwa kwa muda wa wiki moja, hivyo wachezaji wamepewa nafasi ya kwenda majumbani kwao kwa ajili ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.

Hata hivyo kocha mkuu wa timu hiyo, Steve Barker, ambaye amekuwa na mwanzo mzuri tangu kuanza kwa msimu, tayari amerejea Afrika Kusini nyumbani kwake kwa mapumziko mafupi kabla ya kurejea kuendelea na majukumu yake. Uamuzi huo umefanyika wakati Simba ikiwa katika kipindi ambacho imekuwa na ratiba yenye msongamano, ikicheza mechi za Ligi Kuu Bara sambamba na zile za Ligi ya Mabingwa Afrika.

BARK 03

Kabla ya mapumziko hayo, Simba ilikuwa imeendelea na mwendo mzuri katika Ligi Kuu Bara, ikiwa haijapoteza mchezo na ikifanikiwa kushinda mechi sita za mwanzo. Ushindi wa mwisho ulikuwa wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC Septemba 16, matokeo yaliyoifanya ifikishe pointi 18. Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ilianza kwa ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi, kabla ya kushinda tena mchezo wa marudiano kwa mabao 6-1 na kufuzu hatua inayofuata.

Taarifa za ndani ya Simba ziliieleza Mwanaspoti kuwa, mapumziko hayo yamepangwa ili kuwapa wachezaji muda wa kupumzisha miili na akili baada ya kipindi cha mechi nyingi, huku kila mchezaji akitakiwa kuhakikisha anarudi akiwa tayari kwa awamu inayofuata ya mashindano. “Wamepewa wiki moja ya mapumziko, wachezaji wamerudi makwao. Kocha naye amekwenda Afrika Kusini, baada ya hapo watarejea kuanza maandalizi tena,”  kilisema chanzo hicho.

KISA 01

“Baada ya wiki hiyo, wachezaji wanatarajiwa kurejea kambini mwishoni mwa mwezi septemba kuanza maandalizi mapya, huku benchi la ufundi likiwa na kazi ya kuhakikisha mapumziko hayapunguzi kasi ambayo timu imeanza nayo msimu.”

Sio wachezaji wote watakuwa mapumziko kwani wengine watakuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa kuelekea mechi za kirafiki na kufuzu Afcon 2027.