Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashujaa Queens  yatamba na uzoefu

MASHUJAA Pict

Muktasari:

  • Mashujaa inaingia msimu mpya ikiwa na kumbukumbu nzuri ya msimu uliopita, ambapo ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake.

KOCHA wa Mashujaa Queens, Rajabu Bwamkuu amesema uwepo wa wachezaji wenye uzoefu katika kikosi chake ni miongoni mwa mambo yanayoweza kuisaidia timu hiyo kuendelea kuwa na ushindani katika Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu.

Bwamkuu alieleza wachezaji waliopitia mazingira tofauti ya ushindani wana nafasi ya kusaidia timu si kwa uwezo wao pekee, bali pia kwa uzoefu wanaoweza kushirikiana na wenzake.

Miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu katika kikosi hicho ni Maimuna Hamis ‘Mynaco’, Zainabu Hamis na Gelwa Yona, ambao ni sehemu ya kundi la wachezaji ambao mchango wao unaweza kuwa muhimu katika safari ya Mashujaa.

“Ni dalili njema kwetu kucheza na timu ngumu kama JKT Queens na Yanga Princess kumetuonyesha namna gani tunakwenda kuonyesha ushindani kwenye ligi,” amesema Bwamkuu.

Uwepo wa wachezaji wa aina hiyo unampa kocha nafasi ya kujenga kikosi chenye mchanganyiko wa uzoefu na nguvu za wachezaji wengine, jambo linaloweza kuongeza ushindani ndani ya timu na kusaidia kuimarisha muunganiko wa kikosi.

Mashujaa inaingia msimu mpya ikiwa na kumbukumbu nzuri ya msimu uliopita, ambapo ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake.