Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mandeke Jr: Riga ni mwanzo tu, naziota ligi tano Ulaya

RINGO Pict

KIUNGO Mshambuliaji Mtanzania anayekipiga Riga FC ya Latvia, Mandeke Jr amesema kufika hatua ya makundi ya mashindano ya UEFA akiwa na klabu hiyo ni hatua kubwa kwake, lakini amesisitiza bado hajafikia malengo makubwa aliyojiwekea katika safari yake ya soka la kulipwa Ulaya.

Mandeke Jr amesema anafurahia hatua hiyo kutokana na muda mfupi aliokaa tangu ajiunge na Riga na mafanikio hayo yana maana ya kubwa kwake kwa kuwa amekuwa sehemu ya historia ya klabu hiyo baada ya kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya kwanza mwaka huu.

“Kwangu ni hatua nzuri na kubwa na najisikia furaha kuwa katika hatua hii kwa muda mfupi tangu kufika Riga.

Uzuri, hii ni neema ya Mungu, maana huu mwaka ndio nimeingia Riga na huu mwaka ndio kwa mara ya kwanza Riga wanafuzu makundi ya mashindano ya UEFA,” amesema Mandeke Jr.

MANDE 01

Hata hivyo, licha ya mafanikio hayo, mshambuliaji huyo amesema bado ana safari ndefu ya kutimiza ndoto zake, akibainisha kuwa kufika hatua ya makundi ya mashindano ya UEFA ni sehemu tu ya safari yake na si mwisho wa malengo aliyojiwekea katika soka la Ulaya.

Mandeke Jr amesema kuwa moja ya malengo yake makubwa ni kucheza katika ligi tano bora za Ulaya, ambazo ni England, Hispania, Italia, Ujerumani na Ufaransa, huku akitamani pia kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Amesema mafanikio anayoyapata kwa sasa akiwa Riga FC yanampa sababu ya kuamini anaweza kusonga mbele zaidi katika taaluma yake, akitazama hatua hiyo kama mwanzo wa safari yenye matarajio makubwa kuliko alipo sasa.

“Kwangu bado sijatimiza lengo kwa kuwa malengo yangu makubwa ni kucheza ligi tano kubwa za Ulaya na kucheza UEFA Champions League. Ila kwangu ni mwanzo mzuri na naona kuna mwanga uko mbele, Inshaallah,” amesema nyota huyo, akionyesha imani ya kufikia ndoto zake katika soka la kimataifa.