Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makocha wapata hofu ya Kariakoo Dabi

MAKOCHA Pict

Muktasari:

  • Kocha wa zamani wa Simba Roberto Oliveira ‘Robertinho’ aliliambia Mwanaspoti ana tamani kuona timu yake ya zamani ya Simba inashinda lakini hata hivyo Yanga wana kikosi bora.

WAKATI presha ikizidi kupanda kuelekea mchezo wa leo wa dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga, makocha wa zamani wa timu hizo wamegawanyika juu ya timu ipi itashinda mchezo huo.

MAKO 01

Kocha wa zamani wa Simba Roberto Oliveira ‘Robertinho’ aliliambia Mwanaspoti ana tamani kuona timu yake ya zamani ya Simba inashinda lakini hata hivyo Yanga wana kikosi bora.

Robertinho raia wa Brazil amesema ana hasira na Yanga baada ya kumfunga maba 5-1 kwenye mchezo kama huo wa Novemba 5, 2023 lakini hata hivyo wapinzani wao hao wana kikosi chenye wachezaji wenye uzoefu na mechi hizo.

“Simba akishinda nitafurahi sana, nakumbuka niliwafunga na baadaye wakanifunga vibaya mabao matano lakini nadhani itakuwa mechi ngumu kwa timu zote, changamoto kwa Simba ni kwamba Yanga wana timu ambayo ina uzoefu na mechi kama hizo,” amesema Robertinho.

MAKO 02

Wakati Robertinho akiyasema hayo kocha wa zamani wa Yanga Nasreddine Nabi amesema; “Sio rahisi kusema nani atashinda, timu zote zinafundishwa na makocha wazuri na wanaojuana, bahati mbaya sana Yanga ilishinda mechi ya ngao ya jamii hiiitafanya Simba kuja kwa nguvu sana kwenye mchezo huo, Yanga wana timu ambayo ina wachezaji wanaojuana na nimeona wanacheza vizuri wana jiamini,” amesema Nabi.

“Nakumbuka mechi kama hizi kunakuwa na utulivu sana kambini hatua kama hii inawafanya wachezaji kuzingatia zaidi ufundi ndio maana tulikuwa tunaweza kushinda, kama nidhamu kama hiyo inaendelea itakuwa ni faida kwa Yanga.”

MAKO 03

Kocha wa zamani wa Simba na staa wa timu hiyo Abdallah Kibadeni ‘King’ amesema; “Nadhani itakuwa mechi yenye ushindani, nimeona Simba ilikuwa nje ikijiandaa wakati Yanga wakibaki hapahapa, kama wachezaji watafuata walichofundishwa na makocha wao basi tutaona mechi nzuri, siwezi kutabiri nani atashinda lakini naamini tutaona mechi nzuri,” amesema Kibadeni.

“Hizi ni timu kubwa sitegemei kuona wachezaji wakicheza vibaya, wafuate sheria za soka ili timu ndogo ziweze kuiga mazuri yao, watoto watakuwa wanaangalia kipi kinafanyika kwa wakubwa ambao ni wao Simba na Yanga.”

Kocha wa zamani wa Yanga na kiungo wa zamani wa timu hiyo Charles Mkwasa ‘Master’ amesema; “Mara nyingi mechi hizi hakunaga ufundi sana, unaweza kuona matumizi makubwa ya nguvu na mbio, ufrundi mara nyingi unaweza kuuona kwa wachezaji mmoja mmoja, itakuwa ni mechi yenye presha kutokanba na uhitaji wa ushindi kwa timu zote, timu ambayo itapunguza kufanya makosa mengi itaweza kushinda.”

Katika mechi za Dabi ya Kariakoo, Kocha Nasreddine Nabi (Yanga) aliongoza timu yake kwenye mechi 9 za kimashindano, akishinda 4, sare 3, na kupoteza 2, huku akitwaa mataji mawili ya Ngao ya Jamii mbele ya Simba.

Kwa upande mwingine, Kocha Robertinho (Simba) aliongoza timu hiyo kwenye dabi 3 pekee, akishinda 1 (2-0 kwenye ligi), sare 1 (alitwaa Ngao ya Jamii kwa penalti), na kupoteza mara 1 (kipigo cha 5-1 dhidi ya Gamondi). Katika mechi mbili walizokutana ana kwa ana makocha hawa kabla ya Nabi kuondoka nchini, Robertinho aliondoka mbabe kwa kushinda mechi ya Ligi Kuu ya Aprili 2023 kwa mabao 2-0 na kisha kuibuka kidedea kwa matuta kwenye fainali ya Ngao ya Jamii ya Agosti 2023 baada ya suluhu ya 0-0.