Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Takwimu za Simba, Yanga kuelekea Dabi ya Kariakoo

TAKWIMU Pict

Muktasari:

  • Safari hii, Yanga na Simba zinaingia kwenye dabi zikiwa zimecheza mechi sita za Ligi Kuu Bara, huku kila upande ukiwa na jambo la kujivunia na eneo la kulifanyia kazi.

KILA Dabi ya Kariakoo inapokaribia, kelele huwa nyingi nje ya uwanja hususani kwa mashabiki, lakini ndani mara nyingi namba ndizo zinazotoa picha ya timu iliyojipanga vizuri zaidi.

Safari hii, Yanga na Simba zinaingia kwenye dabi zikiwa zimecheza mechi sita za Ligi Kuu Bara, huku kila upande ukiwa na jambo la kujivunia na eneo la kulifanyia kazi.

Kwa upande wa Yanga, hesabu zinaonekana kuvutia zaidi. Mabingwa hao wamecheza kwenye mechi zote sita bila kupoteza wala kutoa sare sawa na Simba, wakikusanya pointi 18, lakini Yanga wakifunga mabao 16 na kuruhusu mawili tu, huku Simba ikifunga 11 na kuruhusu mawili. Hapo ndipo vita ya kwanza ya namba inapoanzia.


TAKWI 02
TAKWI 02

YANGA MOTO MBELE

Ukitazama namba za mabao, Yanga iko mbele. Katika mechi sita imefunga mabao 16, wastani wa kufunga mabao mawili katika kila mechi, tofauti na Simba iliyofunga 11, sawa na wastani wa kufunga bao moja. Tofauti ya mabao matano si jambo dogo kwenye mechi sita. Inaonyesha Yanga imekuwa na uwezo mkubwa wa kubadilisha nafasi inazotengeneza kuwa mabao.

Katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Coastal Union na 4-0 dhidi ya JKT Tanzania, Yanga ilionyesha wazi uwezo huo. Inaweza kushambulia kwa nguvu, kutumia mawinga wake pembeni, kuingia katikati na pia kupata mabao kupitia mipira iliyokufa. Peter Shalulile, Albert Kangwanda, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya na wenzake wameifanya Yanga kufunga mabao kupitia kila engo. Mpinzani akiwadhibiti washambuliaji, bado kuna uwezekano wa kutokea katikati na upande mwingine.


TAKWI 05

SIMBA UKUTA

Simba imeruhusu mabao mawili pekee katika mechi sita, sawa na Yanga. Wote wakiwa hawajaruhusu mabao kwenye mechi nne.

Eneo la mabeki likiongozwa na Rushine De Reuck akishirikiana na Ismail Toure, Nathaniel Chilambo na Antony Mligo au Nickson Kibabage wametengeneza safu bora ya ulinzi na kuifanya dabi isiwe rahisi kutabiri.

Simba imeonyesha uwezo wa kucheza kwa nidhamu na kulinda matokeo. Ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC ndiyo mfano mzuri. Simba haikuwa na umiliki mkubwa, lakini ilitumia nafasi ilizopata kwa ufanisi na kuhakikisha Azam haipati nafasi nyingi za wazi. Hii ni Simba ambayo haionekani kulazimika kumiliki mpira muda wote ili kushinda.


TAKWI 03

UMILIKI MPIRA

Namba nyingine inayovutia ni umiliki wa mpira. Yanga imekuwa na wastani wa takriban asilimia 61.7, wakati Simba ikiwa na asilimia 58.6.

Tofauti si kubwa sana, lakini inaonyesha timu zote zinapenda kuwa na mpira.

Tofauti ipo kwenye namna zinavyoutumia mpira. Yanga mara nyingi inautumia mpira kujenga mashambulizi na kuongeza presha kwenye eneo la mpinzani. Simba nayo inautumia kujenga mchezo, lakini imeonyesha pia uwezo wa kuacha mpinzani awe na mpira kwa muda kisha kumpiga wakati inapofunguka.

Kwenye dabi, hili linaweza kuwa eneo la kuvutia zaidi. Timu itakayolazimisha mchezo kwa masharti yake inaweza kupata faida kubwa.


TAKWI 01
TAKWI 01

MASHUTI

Yanga pia inaongoza kwa wastani wa mashuti. Kwa takwimu za mechi zao sita Yanga inapiga takriban mashuti 12.5 kwa mchezo mmoja, wakati Simba inapiga 11.6.

Hapa ndipo namba ya mabao 16 dhidi ya 11 inakuwa na maana. Yanga inazalisha mashambulizi mengi na imekuwa na ufanisi mkubwa zaidi wa kuyabadilisha kuwa mabao sawa na Simba, lakini inahitaji kuongeza makali katika mwishoni yaani kwenye umaliziaji.

Kwa dabi, hilo linaweza kuwa jambo kubwa. Mechi kubwa mara nyingi hazitengenezwi nafasi nyingi kama mechi za kawaida. Timu inayotumia nafasi mbili au tatu itakazopata inaweza kuibuka na ushindi.


TAKWI 04

UDHAIFU UNAWEZA KUAMUA

Namba nzuri hazimaanishi timu haifanyi makosa.Yanga, licha ya kufungwa mabao mawili tu, imeonyesha wakati mwingine inaweza kupoteza umakini kwenye safu ya ulinzi.

Makosa dhidi ya Namungo na Coastal Union yanaonyesha mawasiliano yakilegea, mpinzani anaweza kupata nafasi. Kadi nyekundu moja kwa Yanga na nne mfululizo kwa Simba katika mechi sita pia ni eneo la tahadhari. Dabi ikiwa na presha kubwa, kucheza pungufu ni hatari ambayo timu haiwezi kuitamani.

Simba kwa upande mwingine, pamoja na ukuta wake imara, imeonyesha wakati mwingine kupata matatizo inaposhambuliwa kwa kasi au inapopoteza mpangilio.

Hivyo, Yanga inaweza kujaribu kulazimisha mchezo wa kasi na kuwavuta mabeki wa Simba kutoka kwenye nafasi zao.


TAKWI 06

DAKIKA 15 ZA MWANZO

Simba imekuwa na udhaifu mkubwa kila baada ya dakika 15 za mwanzoni za mchezo, ikiwa kwenye dakika hizo imekuwa kwenye kiwango kizuri sana na kumiliki mpira kwa nguvu lakini michezo mingi mikubwa wachezaji wa timu hiyo baada ya kupita dakika hizo imekuwa ikishuka taratibu na kuwaachia wapinzani wao waendelee kutawala mchezo.

Kwa upande wa Yanga wamekuwa na wastani mzuri wa kufunga mabao kipindi cha pili hivyo ni timu ambayo inaweza kupambana na mpinzani vizuri endapo itakuwa na ulinzi imara dakika za mwanzo za mchezo huo.