Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makata: Hatuogopi majina ya mastaa Yanga

MAKATA Pict

KOCHA Mkuu wa Polisi Tanzania, Mbwana Makata amewaandaa wachezaji wake kisaikolojia na kimwili kwa ajili ya kuivaa Yanga, akiwataka wasitikiswe na ukubwa wa majina ya wapinzani wao bali waingie uwanjani kupambana na kuhakikisha pointi tatu zinabaki nyumbani.

Polisi Tanzania itakuwa mwenyeji wa Yanga Novemba 20, kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na hali ya timu hizo kwenye msimamo wa ligi.

Polisi inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 11, ikishinda nne, sare tatu na kupoteza nne. Imefunga mabao 13 na kuruhusu 12.

Kwa upande wa Yanga, ina pointi 25 baada ya mechi 10, ikishinda nane, sare moja na kupoteza moja, ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Simba yenye pointi 30.

Akizungumza na Mwanaspoti, Makata amesema kuwa maandalizi yao yamejikita zaidi katika kuwajenga wachezaji kimwili (physical), akiamini kwamba wanahitaji kuwa tayari kukabiliana na kasi, nguvu na ubora wa kikosi cha Yanga.

MAKA 03

Kocha huyo aliwataka wachezaji wake kuondoa hofu ya kukutana na timu yenye majina makubwa, akiwakumbusha kuwa matokeo ya mchezo hayaamuliwi na majina ya wachezaji bali kazi wanayoifanya ndani ya dakika 90.

“Tumekuwa tukijiandaa kwa mchezo huu, hasa kwenye eneo la utimamu wa mwili. Wachezaji nimewaambia wasiiogope Yanga kwa sababu ya ukubwa wa majina yao. Tunachotakiwa kufanya ni kwenda uwanjani na kucheza mpira wetu, kupambana na kuhakikisha tunapata pointi tatu nyumbani,” amesema Makata.

Amesema faida ya kucheza nyumbani ni jambo ambalo wanapaswa kulitumia vizuri, lakini hilo haliwezi kutokea bila nidhamu, kujituma na kutekeleza majukumu yao kwa umakini.

MAKA 02

“Tunaiheshimu Yanga kama timu kubwa, tunajua ina wachezaji wazuri na ina malengo yake, lakini sisi pia tuna malengo yetu. Hatupaswi kuingia uwanjani tukiwa na hofu ya majina yao. Tunahitaji kujiamini na kufanya kazi yetu,” amesema.


MAKA 02

USHARIKA NI NGUVU YA MAKATA

Polisi Tanzania inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kurejea kucheza Uwanja wa Ushirika baada ya kutumia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, kwa mechi zake za nyumbani mwanzoni mwa msimu huu.

Mchezo dhidi ya Pamba Jiji Oktoba 23,2026 ulikuwa wa kwanza kwa Polisi kurejea Ushirika baada ya miaka mitatu na siku 161, tangu mara ya mwisho kucheza hapo Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Tangu kurejea hapo, Polisi imecheza mechi mbili za ligi, ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Pamba Jiji kabla ya kuifunga Geita Gold bao 1-0 Novemba Mosi,2026.

Hivyo, katika mechi hizo mbili za nyumbani Ushirika, Polisi haijapoteza, ikiwa na ushindi mmoja na sare moja, ikifunga mabao mawili na kuruhusu moja, lakini wakati iko Championship haikuwahi kupoteza katika uwanja huo.