Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabula anavyoishi kistaa Algeria

Muktasari:

  • Mabula si tu kwamba amepewa nafasi ya kuonyesha kipaji chake katika moja ya klabu zinazoshiriki soka la ushindani barani Afrika, bali pia anaingia kwenye listi ya mastaa Afrika wanaoishi kifahari.

ACHANA na kiwango bora anachokionyesha kiungo fundi wa Timu ya Tanzania 'Taifa Stars', Alphonce Mabula ndani ya uwanja, kwani maisha anayoyaishi tangu alipojiunga na JS Kabylie ya Algeria ni ya kishua kweli kweli.

Mabula si tu kwamba amepewa nafasi ya kuonyesha kipaji chake katika moja ya klabu zinazoshiriki soka la ushindani barani Afrika, bali pia anaingia kwenye listi ya mastaa Afrika wanaoishi kifahari.

Kuanzia mshahara mnono, nyumba ya kisasa, gari kali, usafiri wa ndege na huduma nyingine. Ni kifurushi kinachoonyesha namna thamani ya wachezaji wa Tanzania inavyozidi kupanda kimataifa, huku safari ya kucheza soka nje ya nchi ikiendelea kuwa fursa ya kubadilisha maisha ya wachezaji wanaopata mikataba mikubwa.


MABU 03

MKATABA WA SH2.3 BILIONI

Mabula amesaini mkataba wa miaka miwili na JS Kabylie, anatarajiwa kuvuna jumla ya Sh2.3 bilioni ikiwa ni mshahara wake na posho za kawaida katika kipindi chote cha mkataba huo.

Kwa hesabu hiyo, kiungo huyo atalipwa takribani Sh1.15 bilioni  kwa mwaka, huku kila mwezi akiingiza Sh95.8 milioni kabla ya kuhesabu bonasi mbalimbali anazoweza kupata kutokana na kiwango chake binafsi na mafanikio ya timu.

Hiyo ni fedha inayomuweka kwenye kundi la wachezaji wenye mikataba yenye thamani kubwa, hasa ukizingatia kuwa kiasi hicho ni mshahara pekee na hakijajumuisha thamani ya huduma nyingine alizowekewa na klabu.


MABU 02

NYUMBA YA KISHUA

Moja ya vitu vinavyoufanya mkataba wa Mabula kuwa wa kuvutia ni nyumba aliyowekewa na klabu hiyo.

Si nyumba ya kawaida, bali ni nyumba ya kifahari yenye vyumba vitatu vya kulala, sebule na vyoo vitatu, huku ikiwa na huduma za ziada zikiwemo bwawa la kuogelea (swimming pool) na gym kwa ajili ya mazoezi yake binafsi.

Thamani ya upangishaji wa nyumba hiyo ni takribani dola 3,000 kwa mwezi, sawa na Sh7.9 milioni kwa fedha za Kitanzania.

Hiyo ina maana kuwa kwa mwaka mmoja, thamani ya makazi hayo inafikia karibu Sh95 milioni, huku kwa kipindi chote cha miaka miwili cha mkataba wake ikifikia takribani Sh190 milioni.


MABU 04

GARI AINA YA JETOUR

Mbali na nyumba klabu hiyo imemnunulia gari aina ya Jetour Traveller T2 XWD ambayo inakadiriwa kugharimu kati ya TSh110 milioni  hadi 150milioni.

Hii ni sehemu nyingine ya kifurushi kinachoonyesha namna klabu hiyo ilivyojipanga kumuweka Mabula katika mazingira mazuri ya maisha na kazi.

Hivyo, mbali na mshahara na makazi, Mabula pia ana uhakika wa usafiri binafsi anapokwenda mazoezini, kwenye mechi na hata anapotoka binafsi ana uhakika wa usafiri.


MABU 05

TIKETI ZA NDEGE, BIMA

Kipengele hicho kinamhakikishia usafiri wa ndege kwa safari zinazohusiana na majukumu yake, ikiwemo anapohitajika kujiunga na Taifa Stars, pamoja na safari zake binafsi kwa mujibu wa makubaliano yaliyowekwa.

Hii ina maana hata anapopata mwaliko wa timu ya taifa, hana presha ya kutafuta fedha za tiketi ili kuwasili kambini na kuungana na wenzake.

Vilevile, klabu hiyo imejumuisha bima ya afya katika mkataba wake, jambo linalompa ulinzi zaidi anapokuwa akitekeleza majukumu yake ya soka nchini Algeria.


MABU 01

BONASI NAZO

Mbali na mshahara wa kawaida, nyumba, gari na huduma nyingine, Mabula anapewa bonasi zinazoweza kuongeza kipato chake.

Bonasi hizo zinahusishwa na malengo na masharti yaliyowekwa na klabu, hivyo endapo atatimiza vigezo vinavyohitajika, ana nafasi ya kuvuna fedha zaidi ya mshahara wake wa kawaida.

Tambua kwamba kila Mabula atakapoonyesha kiwango bora basi ana uhakika wa kuvuna bonasi kutoka kwa timu.