Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samatta, Novatus walivyokiwasha Ulaya

SAMATTA Pict

Muktasari:

  • Kiungo fundi Alphonce Mabula naye wikiendi iliyopita alikuwa na kiwango bora akicheza dakika 65 chama lake la JS Kabylie likiondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya El Biar kwenye ligi Kuu Algeria.

WIKIENDI hii imekuwa ya kuvutia kwa wachezaji wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, huku wakionesha viwango vya juu na kuacha alama katika timu zao kwenye mashindano mbalimbali Ulaya na kwingineko.

Mshambuliaji na nahodha wa zamani wa timu ya taifa, Mbwana Samatta alionyesha ubora mkubwa alipoingia uwanjani akitokea benchi wakati chama lake Le Havre F.C ilipokuwa nyuma kwa mabao 4-1.

Licha ya ugumu wa mchezo huo na timu yake kuwa nyuma kwa idadi kubwa ya mabao, Samatta alionyesha mabadiliko ya haraka ndani ya dakika 25 tu alizocheza uwanjani, akipiga mashuti matatu na mawili kati yake yalikwenda kulenga lango.

SAM 01

Samatta ambaye aliacha alama kubwa kwenye soka la Ulaya akitumikia ligi mbalimbali ikiwemo Fenerbance, Aston Villa, Royal Antwerp huu umekuwa msimu wake wa pili kuitumikia Le Havre akifunga mabao mawili kwenye mechi tisa.

Msimu uliopita kwenye mechi 27 alifunga idadi hiyo ya mabao na asisti moja.

Kwa upande mwingine, kiungo Novatus Miroshi alikuwa na siku nzuri kazini alipokuwa na kikosi chake kilipocheza dhidi ya Fenerbahce kwenye Ligi Kuu ya Uturuki (Super Lig), akianza katika kikosi cha kwanza na kumaliza dakika 90 kabla ya kufanyiwa mabadiliko dakika za nyongeza.

Novatus alionyesha kiwango bora uwanjani takwimu zinaonyesha alipiga pasi 51 zenye usahihi wa asilimia 67 na asilimia 85 katika eneo la mwisho, sambamba na kupokonya mipira mitano na kuzuia shuti moja la hatari.

SAM 02

Kiwango hicho kilimfanya amalize mchezo huo kwa alama ya juu ya 7.3, kiwango kilichomfanya kuwazidi wachezaji wengine maarufu akiwemo Ngolo Kante aliyetoka na alama 7.0 katika mchezo huo uliomalizika kwa Goztepe F.C kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fenerbahce.

Kiungo fundi Alphonce Mabula naye wikiendi iliyopita alikuwa na kiwango bora akicheza dakika 65 chama lake la JS Kabylie likiondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya El Biar kwenye ligi Kuu Algeria.