Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabaharia wang’oa nanga ZPL

MABAHARIA Pict

Muktasari:

  • Ushindi huo umeifanya KMKM kutoka mwishoni mwa msimamo wa ligi hiyo hadi kufika nafasi ya 10 ikiwa na pointi saba ikifunga mabao sita sawa na waliyoruhusu. Timu hiyo ilipata ushindi wa kuifunga bao 1-0 JKU kisha BlackSailors 2-0.

MABAHARIA wa KMKM wameanza kuwa imara ndani ya Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), baada ya kushinda mechi mbili mfululizo dhidi ya JKU na BlackSailors.

Ushindi huo umeifanya KMKM kutoka mwishoni mwa msimamo wa ligi hiyo hadi kufika nafasi ya 10 ikiwa na pointi saba ikifunga mabao sita sawa na waliyoruhusu. Timu hiyo ilipata ushindi wa kuifunga bao 1-0 JKU kisha BlackSailors 2-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, kiungo wa timu hiyo, Imran Mohammed Abdallah ‘Jaba’ amesema kufanya vibaya michezo minne ya kwanza ilitokana na uchovu wa maandalizi ya michezo ya kimataifa.

Jaba amesema ushindi wa michezo miwili umeirudisha kasi na motisha kikosini kuendelea kupambana katika mechi zilizobaki za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

Amesema, wataendelea kupambana kuhakikisha muendelezo wa matokeo mazuri unakuwepo katika michezo tisa iliyobaki ya duru la kwanza kuhakikisha hawamalizi ligi vibaya.

“Kwa kweli tumeanza ligi vibaya msimu huu kwani tumepitia kipindi kigumu ambacho hatupo tayari kurudi tena tulipotoka,” amesema.

Kiungo huyo amesema kwasasa wapo kwenye maandalizi ya kuikabili Muembe Makumbi City Oktoba 10, 2026 kwenye uwanja wa Mao A uliopo Unguja, hivyo watahakikisha wanaendeleza matokeo mazuri.