Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabadiliko ya Kombe la Mapinduzi 2027

MAPINDUZI Pict

Muktasari:

  • Hii haitakuwa mara ya kwanza Kombe la Mapinduzi kuchezwa kwa mfumo wa timu za taifa, kwani mwaka 2025 lilishirikisha timu nne,  Kilimanjaro Stars, Kenya, Burkina Faso na wenyeji Zanzibar Heroes, kama sehemu ya maandalizi ya CHAN.

RATIBA ya mashindano ya klabu barani Afrika, imeonekana kuwa sababu kubwa ya kubadilishwa kwa mfumo wa Kombe la Mapinduzi 2027, huku Simba, Yanga, Azam na Singida Black Stars zikitarajiwa kukosekana kutokana na ushiriki wao katika hatua ya makundi ya michuano ya CAF.

Hatua ya makundi ya mashindano hayo inatarajiwa kuanza Novemba 27, 2026 na kuendelea hadi Januari 24, 2027, kipindi ambacho kinagongana na muda wa kuchezwa kwa Kombe la Mapinduzi ambalo huchezwa mwishoni mwa Desemba na tamati yake huwa Januari 13 ya kila mwaka.

Hali hiyo inamaanisha klabu hizo nne, ambazo zinaiwakilisha Tanzania katika mashindano ya CAF, zitakuwa na majukumu ya kimataifa, hivyo kushindwa kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa mfumo wa kawaida wa klabu.

Taarifa ilizonazo Mwanaspoti zinaeleza, kutokana na mazingira hayo, Kombe la Mapinduzi 2027 linatarajiwa kuchezwa kwa mfumo wa timu za taifa, kama ilivyofanyika mwaka 2025. Mfumo huo unaweza kuzipa nafasi Simba, Yanga, Azam na Singida Black Stars kuelekeza nguvu zao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, huku Kombe la Mapinduzi likiendelea kutoa burudani kwa mashabiki kwa muundo tofauti.

Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, tayari imethibitisha kuwa michuano hiyo itachezwa, ingawa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu mfumo kamili utakaotumika.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mattar Zahor Massoud, amesema kuna baadhi ya mambo ambayo wizara inaendelea kuyafanyia kazi kabla ya kutangaza rasmi ratiba na mfumo wa michuano hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Migombani kisiwani Unguja, Mattar amesema Kombe la Mapinduzi la mwaka huu litakuwa tofauti na lilivyokuwa mwaka uliopita.

“Kombe la Mapinduzi litachezwa, lakini mwaka huu tumebadilisha mfumo. Hautakuwa kama ilivyokuwa mwaka uliopita,” amesema Mattar. Katibu huyo aliwataka mashabiki na wadau wa michezo kuwa na subira huku wakisubiri taarifa rasmi na wizara inaendelea na maandalizi ili kuhakikisha michuano hiyo inakuwa na ushindani na burudani kwa wananchi.

Hii haitakuwa mara ya kwanza Kombe la Mapinduzi kuchezwa kwa mfumo wa timu za taifa, kwani mwaka 2025 lilishirikisha timu nne,  Kilimanjaro Stars, Kenya, Burkina Faso na wenyeji Zanzibar Heroes, kama sehemu ya maandalizi ya CHAN.