Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maajabu ya ‘Red’ Yanga, TRA United

MAKUND 08

Muktasari:

  • Katika mechi zilizochezwa kwenye uwanja huo, imeshuhudiwa kila timu ikitoa mchezaji mmoja aliyeonyeshwa kadi nyekundu kwa msimu wa pili mfululizo, huku matokeo pia yakiendelea kumalizika kwa suluhu (0-0).

MECHI ya Ligi Kuu Bara kati ya TRA United dhidi ya Yanga iliyopigwa Oktoba 24, 2026 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini, Arusha na kuisha suluhu (0-0), imeendeleza majaabu kwa miamba hiyo, ikiwa ni msimu wa pili mfululizo.

Katika mechi zilizochezwa kwenye uwanja huo, imeshuhudiwa kila timu ikitoa mchezaji mmoja aliyeonyeshwa kadi nyekundu kwa msimu wa pili mfululizo, huku matokeo pia yakiendelea kumalizika kwa suluhu (0-0).

Msimu wa 2025-2026, katika mechi iliyochezwa hapo Machi 18, 2026, iliisha suluhu (0-0), huku kiungo nyota wa TRA United, Mzamiru Yassin akionyeshwa kadi nyekundu, baada ya kumchezea madhambi beki, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

Mzamiru alionyeshwa kadi hiyo iliyotokana na kadi mbili za jano dakika ya 76, hata hivyo Yanga ilishindwa kutumia nafasi ya wapinzani kuwa pungufu kupata bao la ushindi na mechi kuisha suluhu (0-0).

Rekodi hiyo imejitokeza tena msimu wa 2026-2027, katika mechi iliyopigwa uwanjani hapo Oktoba 24, 2026 na kuisha kwa suluhu (0-0), huku kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya akionyeshwa pia kadi nyekundu.

Katika mechi hiyo, Mudathir alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90+1 baada ya kumzuia kiungo mshambuliaji wa TRA United, Abdulhamid Juma aliyekuwa akienda kufunga, huku kiungo huyo wa Yanga akiwa ni mchezaji wa mwisho.

Kwa maana hiyo, katika mechi ya msimu uliopita wa 2025-2026 na 2026-2027, ambao timu hizo zimekutana zimetoka suluhu (0-0), huku ikishuhudiwa kila mchezaji wa pande zote akionyeshwa kadi nyekundu, ikionyesha ushindani pindi zinapokutana.