Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lionel Messi aiongoza Argentina kuizamisha Timu ya Brazil

Muktasari:

KATIKA toleo lililopita mwandishi Luca Caiola alituonyesha jinsi Messi alivyoibuka katika timu ya vijana ya Argentina hadi kocha akawa anaulizwa alipomtoa mchezaji huyo hasa kwa namna alivyowashangaza mashabiki kwa soka la uhakika. Endelea…

KATIKA toleo lililopita mwandishi Luca Caiola alituonyesha jinsi Messi alivyoibuka katika timu ya vijana ya Argentina hadi kocha akawa anaulizwa alipomtoa mchezaji huyo hasa kwa namna alivyowashangaza mashabiki kwa soka la uhakika. Endelea…

“Aliniuliza nilimtoa wapi huyo kijana, aliamini alikuwa vizuri, vipi utamuanzisha tangu mwanzo katika mechi ijayo dhidi ya Uruguay?” Aliniuliza.

Hapana. Katika mechi na Uruguay mjini Colonia, Messi hakuwamo katika kikosi cha kwanza lakini anapoingia tu anamshangaza kila mtu. Siku iliyofuata yaani Jumapili ya Julai 4, jarida maarufu la michezo la mjini Buenos Aires linaloitwa ‘Ole’ liliandika, ‘Messi ni mpango wa uhakika’. Alifunga mabao mawili na kutoa pasi nne na kushuhudia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Uruguay.

Mechi mbili za kimataifa za Messi ziliwavutia, na kuanzia hapo Tocalli akawa hana hofu kumpa nafasi katika kikosi chake kilichokwenda Marekani ya Kusini kwa ajili ya mashindano ya vijana kuwania kufuzu kucheza fainali za dunia za Fifa kwa vijana chini ya miaka 20 zilizopangwa kuchezwa Januari ya mwaka uliofuata.

Mashindano hayo yalifanyika nchini Colombia na timu ya Argentina ilipata tabu kuendana na mazingira ya hali ya hewa lakini kiujumla Messi hakupewa nafasi na kocha wake katika mashindano hayo zaidi ya muda mfupi aliocheza tena katika kila kipindi cha pili na Tocalli alieleza ni kwa nini ilikuwa hivyo.

“Huo ni uamuzi wangu, kijana huyu bado hajazowea aina ya uchezaji wa timu hii, amezowea ligi a vijana akiwa na Barca, hakuwa na kasi ile ile ambayo ingemfaa kucheza katika mazingira ya hali ya hewa ya Marekani ya Kusini.

“Ni mechi zilizokuwa na kila aina ya ushindani na zaidi ya hilo wapinzani wake wengi wao wanamzidi miaka miwili, ni tofauti kubwa, kwa hiyo niliamua kumtumia kwa uangalifu ili asije akaumia au kubebeshwa majukumu mengi.

Ni mbinu ambayo baadaye ililipa, Messi alifunga mabao matano na kushika nafasi ya pili ya ufungaji bora katika mashindano hayo huku Argentina ikishika nafasi ya tatu nyuma ya Colombia na Brazil waliobeba taji.

Kwa matokeo hayo maana yake ni kwamba Argentina walifuzu kucheza fainali za dunia kwa vijana chini ya miaka 20 ambazo zilipangwa kufanyika nchini Uholanzi. Mashindano hayo yalipangwa kuanza Jumamosi ya Juni 11, 2005 na mechi ya kwanza ya Argentina ilikuwa ni dhidi ya Marekani, kwa mshangao wa mashabiki, Messi hakuwamo katika kikosi cha kwanza na Argentina ikalala kwa bao 1-0.

Huo ulikuwa mwanzo mbaya katika mashindano hayo lakini Messi alimfanya kila mtu aendelee kuwa katika hali ya utulivu, “niko poa kifikra nafikiri niko sawa kucheza kwa dakika 90 lakini natakiwa kuheshimu uamuzi wa kocha,’’ alisema.

“Timu itakuwa katika kasi ya mchezo kwa sababu tuna wachezaji wazuri tuna kila kitu cha kutuwezesha kufuzu,’’ aliongeza. Messi alikuwa sahihi na katika mechi na Misri iliyochezwa Juni 14 alidhihirisha hilo.

Safari hii alikuwa katika kikosi cha kwanza, alifunga bao la kwanza na kuidhoofisha timu ya Misri na kumfanya Zabaleta amalizie kwa bao la pili. Mechi ya tatu ilikuwa ni dhidi ya Ujerumani na hii kidogo ilikuwa mtihan, ilikuwa ni mechi ambayo ingeamua timu ipi iende hatua ya 16 bora, Ujerumani walikuwa na pointi moja zaidi ya Argentina, hivyo sare iliwatosha ili kusonga mbele.

Katika mechi hiyo Messi alidhihirisha ubora wake, aliunasa mpira katikati ya uwanja akawapita mabeki kabla ya kutoa pasi ya uhakika, Oberman akafanya kama kuupisha mpira huo na ukamkuta Neri Cordoso aliyeipatia bao Argentina na kufanya matokeo yasomeke 1-0. Katika mechi zilizofuata waliichapa Colombia mabao 2-1 na kuichakaza Hispana mabao 3-1. Katika nusu fainali walikutaba na Brazil, mechi iliyozikutanisha timu ambazo zimewahi kutwaa taji hilo mara nne, katika dakika nane za awali, Argentina tayari walikuwa wameutawala mchezo na kupata bao la kwanza lililofungwa na Messi kwa mkwaju wa mbali uliomshinda kipa wa Brazil.

Hata hivyo Renato aliisawazishia Brazil katika kipindi cha pili lakini katika dakika za majeruhi Zabaleta aliunasa mpira uliombabatisha beki wa Brazil na kufanikiwa kuongeza bao la pili kwa Argentina. Hadi hapo Argentina ikawa inasubiri mechi ya fainali Julai 2, 2005 kwenye Uwanja wa Galgenwaard, wapinzani wao walikuwa ni Nigeria ambao waliifunga Morocco katika mechi nyingine ya nusu fainali.

Itaendelea Jumamosi ijayo…