Linah kukoleza mahaba kwa mpenzi wake
Dar es Salaam. Mwanamuziki Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa yuko tayari kuongeza mtoto mwingine na mpenzi wake ajulikanaye kwa jina la Mchomvu.
Linah amesema kutokana na kuwa na mapenzi ya dhati kwa mpenzi wake, yupo tayari kufanya mchakato wa kumtafuta mdogo wa Tracey.
Amesema pia, kuzaa mapema na kumaliza ndiyo poa ili aweze kuendelea na kazi zake vizuri kuliko kukaa muda mrefu halafu ndiyo ubebe ujauzito tena.
“Niko tayari sasa hivi kumzalia Mchomvu mtoto mwingine, kutokana na kunionyesha mapenzi ya dhati na mimi pia nampenda sana, hivyo msije shangaa siku mkiniona mjamzito tena maana ni maamuzi ninayoamua.
"Kwanza ndiyo furaha yetu kubwa kuwa na watoto wengi na kitu kingine tukizaa haraka ni vizuri zaidi tunaweza kufanya kazi zetu kwa ajili ya kusomesha na si kufikiria kuzaa tena,” alisema Linah Sanga.