Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kusah: Ruby hanilei, tunaleana

Muktasari:

Mpenzi wa Ruby apinga madai ya kulelewa na amesema yeye ndio mwandishi wa nyimbo zake na wapo wote tangu apotee kwenye anga ya muziki.

MZAZI mwenzie msanii Ruby, Salmin Ismail anayejulikana kwa jina la Kusah, amesema halelewi na msanii huyo.
Kusah amesema wengi hawaelewi na hawamjui vizuri  Ruby hadi anapanda jukwaani kwa nyimbo zake nani anakuwa amesababisha.
“Nawasemehe wote wanaosema mimi nalelewa na Ruby sababu najua hawajui kinachoendelea katika maisha ya muziki ya Ruby, mimi ni mwandishi wa nyimbo za Ruby karibia nyingi ukiachana na wimbo wake wa Ntande, Alele nilizomuandikia zinapendwa na watu, pia hata shoo nyingi mimi ndio natafuta sasa watu wanasemaje mimi nalelewa?
“Au kwakuwa namuweka mbele Ruby mie nipo nyuma yake? na wajue tu nipo na Ruby tangu alipopotea katika muziki na yote hiyo ni tunachakarika ili tupate kuishi maisha mazuri na ukizingatia tumepata mtoto ndio familia hiyo, naomba watu waache kuzungumza maneno yasiyo na uhakika” anasema Kusah
Kusah ni mwandishi wa nyimbo na pia ni mwanamuziki, wameingia kwenye uhusiano wa mapenzi na Ruby kwa muda mrefu hadi sasa wamepata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Aliya.