Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kondo akabidhiwa mikoba Bandari Tanzania

KONDO Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo inayomilikiwa na Mamlaka ya Bandari nchini, ilimaliza msimu uliopita wa First Legue kibabe ikiwa nafasi ya kwanza kundi A kwa pointi 32 na kufanikiwa kupanda daraja na msimu ujao itacheza Championship kuisaka Ligi Kuu.

BAADA ya kupanda Championship, Bandari Tanzania imesema mkakati wake ni kucheza Ligi Kuu, ikijivunia usajili wa nyota wenye uwezo na uzoefu wa soka la ushindani, huku ikimkabidhi jukumu Habibu Kondo kuwa Kocha Mkuu.

Timu hiyo inayomilikiwa na Mamlaka ya Bandari nchini, ilimaliza msimu uliopita wa First Legue kibabe ikiwa nafasi ya kwanza kundi A kwa pointi 32 na kufanikiwa kupanda daraja na msimu ujao itacheza Championship kuisaka Ligi Kuu.

Hadi sasa timu hiyo imeshatangaza kuachana na nyota wake 14 wakiwa ni Hamad Ally, Sweetbert Amrima, Hamad Manzi, Amir Ulanga, Bryan Hizza, Ronaldo Matozi, Ismail Siad na James Kahimba.

Wengine ni Salum Kika, Said Dihon, Nassor Ngwale, Gitu Sakka na Paschal Kibandula, huku ikiwanasa Hajji Ugando, William Gallas, Nassor Kapama, Isah Ngoah, Nizar Abdalah na Ayoub Nassor kutoka.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Ismail Chimpele amesema ili kufikia malengo yao, wameanza na uboreshaji wa benchi la ufundi kwa kumpa Kondo kuwa kocha mkuu akisaidiana na Omega Seme aliyeipandisha daraja.

Kuhusu usajili wa wachezaji, kigogo huyo amesema wanatarajia kuwa na sura mpya 20 ambapo kwa sasa wanaendelea na maandalizi akieleza kuwa uongozi umejipanga kufikia ndoto zao na kuwapa raha mashabiki wake.

“Tunashukuru kwa sapoti ya wadau wetu tangu tulipoanza msimu uliopita hadi kufanikisha kupandisha timu, kwa sasa kazi iliyobaki ni kuendeleza yale ya msingi kupanda Ligi Kuu, hii ndio lengo letu”  amesema Chimpele.

Amesema wameamua kuwa na kikosi bora na imara kutokana na ligi wanayotarajia kushiriki kuwa na ugumu, akieleza kuwa muda wowote timu itaanza kambi kujiandaa na ligi hiyo msimu ujao.

“Championship tunaijua ilivyo ngumu ukizingatia na wapinzani tulionao si wa kubeza, timu itaingia kambini muda wowote na tunatarajia kuwa Zanzibar tukiamini ni sehemu nzuri kwetu, kimsingi tumepania Ligi Kuu”ametamba bosi huyo.