Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Mwandila: Yanga tunapindua meza kwa Gor Mahia

Muktasari:

Yanga haijashinda mechi yoyote katika Kundi D ikiwa inashikilia mkia

Dar es Salaam. Kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amesema kikosi na maandalizi waliyofanya yanatosha kuwafunga Gor Mahia na kupindua matokeo ya mechi ya kwanza.

Yanga walifungwa 4-0, Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Kasarani, Nairobi watarudiana kesho kwenye Uwanja wa Taifa katika mechi ya Kundi D.

Mwandila alisema kuongezeka kwa baadhi ya wachezaji ambao walikosekana katika mechi ya kwanza wataongeza nguvu katika timu hiyo.

Alisema tunakiu ya kupata ushindi wa kwanza baada ya kucheza mechi tatu bila ushindi na kushindwa kufunga hata bao.

"Kama benchi la ufundi tumejipanga na kufanya maandalizi ya kutosha ili kucheza katika kiwango kizuri tena tukiwa nyumbani na kushinda kwani hilo ndio lengo letu kuu," alisema Mwandila.

"Hatukuwa imara katika mechi za mwanzo kwani tulikuwa tukifanya makosa mengi lakini tumeyaona na kuyarekebisha hayo na jukumu limebaki kwa wachezaji, " alisema Mwandila.

Nahodha wa Yanga, Juma Abdul alisema  wachezaji wenzake wote wanamorali ya hali ya juu ili kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi.

"Kuanzia kambini mpaka mazoezi kila mchezaji yupo na hali na morali kuhakikisha tunashinda kwa mara ya kwanza tukiwa nyumbani," alisema Abdul.