Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Burundi: Ushindi umetupa mwanzo mzuri

Muktasari:

  • Burundi ilianza kwa ushindi mnono katika mchezo huo wa Kundi C uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, huku Amini Nshimirimana akifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na kuiweka timu yake kwenye nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi.

KOCHA Mkuu wa Burundi, Jean De Dieu Rukundo, amesema ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Sudan Kusini umeipa timu hiyo mwanzo mzuri katika kampeni za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 (AFCON U-20).

Burundi ilianza kwa ushindi mnono katika mchezo huo wa Kundi C uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, huku Amini Nshimirimana akifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na kuiweka timu yake kwenye nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi.

Baada ya mapumziko, mchezo huo ulilazimika kusimama kwa takribani dakika 30 kutokana na hali ya hewa, lakini baada ya kuendelea Burundi iliendelea kuonyesha nguvu na Sympathque Majidi akafunga mabao mawili yaliyokamilisha ushindi wa mabao 4-0.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Rukundo alisema anafurahishwa na namna kikosi chake kilivyoanza mashindano, akiamini ushindi huo utawapa morali ya kuendelea kupambana katika michezo inayofuata.

“Ninafurahi sana na ushindi huu mkubwa kwa sababu umetupa mwanzo mzuri kabisa kwenye mashindano tunajua mbeleni tuna kibarua dhidi ya Kenya ambayo ni timu nzuri sana,” alisema Rukundo.

Kocha huyo alisema matokeo hayo yanawapa nafasi ya kuanza safari yao ya mashindano wakiwa na hali nzuri, huku akitazama michezo inayofuata kama sehemu ya kuendeleza kasi waliyoianza dhidi ya Sudan Kusini. Ushindi huo umeifanya Burundi kuanza kampeni zake kwa pointi tatu na mabao manne.