Kisa dabi! Washindi Betika watambiana
Wakati mashabiki wakihesabu saa kuona nani ataondoka na pointi tatu keshi kwenye dabi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, mashabiki wa timu hizo wametambiana kila upande ukijinasibu ushindi.
Mashabiki hao ambao ni washindi wa Betika Mtoko wa Kibingwa msimu huu wametambiana kila upande ukijinasibu kupata matokeo mazuri kwenye dabi hiyo ya raundi ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Mashabiki 50 wa Betika Mtoko wa Kibingwa msimu huu wataishuhudia mubashara dabi hiyo kwa gharama za Betika.
Wakizungumza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege ya Dar es Salaam leo asubuhi, mashabiki wa timu hizo mbili kila mmoja alimtambia mwenzake kushinda kesho huku wale wa Yanga wakisema hakuna mchezaji wanayemhofia Simba.
"Kipigo kiko pale pale, Mnyama atachinjwa, hilo halina ubishi," amesema Michael Marius wa Rukwa ambaye ni shabiki kindakindaki wa Yanga.
Shabiki mwingine, Mgasa Wambura wa Tarime amesema Yanga haiwezi kukubali 'uteja' kwa Simba na leo ushindi ni lazima Jangwani.
"Aziz Ki lazima atupie, hilo halina ubishi," amesema.
Juma Makaranga kutoka Mtwara ambaye ni mnazi wa Simba alitabiri sare ya 1-1 akidai Yanga itacheza kwa presha zaidi.
"Sisi Simba tutacheza mpira, wenzetu naona namna watakavyokamia, japo namhofia sana Max, ni mchezaji mzuri na atatusumbua, lakini mwisho wa yote tusubiri dakika 90," amesema.
Mshindi mwingine, Pius Stephano kutoka Manyara
ambaye yeye si Simba wala Yanga lakini anapenda soka anasema yoyote itakayeshinda kwake fresh.
Washindi hao wataishuhudia laivu dabi hiyo, wengine ikiwa ni mara yao ya kwanza kwa udhamini wa Kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya Betika.
Ofisa habari wa kampuni hiyo,
Rugambwa Juvenalius amesema washindi hao wa promosheni ya Betika Mtoko wa Kibingwa msimu huu wamewasili Dar es Salaam.
"Wataungana na wenzao wa Dar es Salaam leo ambapo watalala kwenye hoteli ya nyota tano na kesho wakiongozwa na king'ora watakwenda Lupaso (Uwanja wa Mkapa) kuishuhudia dabi kwa hadhi ya VIP kesho,".
Amesema kama kauli mbiu yao ya
Shinda bila miyeyusho, Betika imeendelea kuthibitisha uimara wake kwa wateja wake.
"Tayari mkeka wa dabi yavSimba na Yanga upo, ni fursa nyingine kwa mashabiki kubashiri na kushinda," amesema.