Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipa Azam afariki dunia kwa ajali ya Pikipiki

KIPA Pict

Muktasari:

  • Ajali za bodaboda zimeendelea kuwa tishio kwa taifa na kwa vijana ambapo takwimu za Ripoti ya Matukio ya Usalama Barabarani ya mwaka 2024, pikipiki zilihusika katika ajali 2,799 mwaka huo.

Kipa wa timu ya vijana chini ya miaka 20 (U-20) ya Azam FC, Iddy Salim, amefariki dunia baada ya kupata ajali ya bodaboda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Azam FC leo Ijumaa Septemba 11, 2026 imesema kipa huyo alifariki dunia jana katika ajali hiyo.

“Tunasikitika kutangaza kifo cha kipa wetu wa timu ya vijana ‘U-20’, Iddy Salim, aliyefariki dunia kwa ajali ya pikipiki jana Alhamisi,” imesema sehemu ya taarifa ya klabu hiyo.

Klabu hiyo imesema mwili wa Iddy kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala (MRRH), Dar es Salaam, ambako unaendelea kufanyiwa taratibu za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Tanga kwa ajili ya mazishi.

“Kwa sasa mwili wa marehemu upo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala (MRRH), kwa ajili ya kufanyiwa taratibu za mwisho kabla ya kusafirishwa nyumbani kwao Tanga kwa ajili ya maziko,” taarifa hiyo imeeleza.

Klabu hiyo imeungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu, huku ikitoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Iddy Salim.

Azam FC imewaomba wadau wa soka na wote walioguswa na msiba huo kuwa pamoja na familia katika kipindi cha majonzi, huku ikitoa pole na kuwatakia nguvu na uvumilivu.