Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinda Mtanzania amkosha Gamondi

KINDA Pict

Muktasari:

  • Hamisi, ambaye anakipiga katika kikosi cha Al Ain U23, amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu wa 2026/27, akicheza mechi nne sawa na dakika 360, huku akiruhusu bao moja pekee na kumaliza michezo mitatu bila nyavu zake kutikiswa.

KWA mara ya kwanza kipa chipukizi wa Tanzania, Abdallah Hamisi anayekipiga Al Ain ya Falme za Kiarabu ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa Taifa Stars kitakachoingia kambini kwa mechi mbili za kufuzu AFCON dhidi ya Nigeria zitakazopigwa Novemba 13 na 17, 2026.

Hamisi, ambaye anakipiga katika kikosi cha Al Ain U23, amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu wa 2026/27, akicheza mechi nne sawa na dakika 360, huku akiruhusu bao moja pekee na kumaliza michezo mitatu bila nyavu zake kutikiswa.

Kiwango hicho kimemfanya Kocha wa Taifa Stars, Miguel Gamondi kuvutiwa na ubora wake akiungana na makipa wengine wawili, Aishi Manula na Zuberi Foba kutoka Azam na wamekuwa wakiitwa mara kwa mara.

KIN 01

Kiwango hicho kimekuja wakati Al Ain U23 kikiendelea kufanya vizuri katika mashindano ya vijana na kilikuwa kileleni mwa msimamo baada ya kushinda michezo yote sita, kikiwa kimefunga mabao 16 na kuruhusu matatu pekee, jambo linaloonyesha uimara wa safu yake ya ulinzi.

Miongoni mwa uwezo alionao kipa huyo ni kuanzisha mashambulizi kutokea chini na uwezo wa kuokoa timu katika mazingira magumu kwa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati.

Kipa huyo kabla ya kuitumikia Al Ain aliwahi kukipiga Fair Play Academy hapa ndipo alipokuwa akipata malezi ya awali ya soka.

Kisha baadae alikipiga Sahare All Stars akiwa kipa wa U-15 kabla haijaitumikia Simba U17, ambako aliendelea kukuza uwezo wake katika kikosi cha vijana cha Simba.

KIN 02

Msimu wa 2019/20 aliichezea African Sports iliyokuwa Daraja la Kwanza. Hapa ndipo alipata nafasi ya kufanya majaribio yaliyompeleka Falme za Kiarabu.

Baada ya kuitumikia Al Ain msimu wa 2022/23 baadae aliitumikia MAJD FC msimu wa 2024/25 na alicheza mechi 26, akiruhusu mabao 36 na kupata clean sheet tatu.

Meneja wa kipa huyo, Mansour Alawi aliwahi kusema "Ameonyesha kiwango cha kuongezeka kila siku, ndiyo maana makocha wakaona anastahili nafasi kwenye timu ya wakubwa na hata timu ya Taifa."

"Upo uwezekano siku zijazo akaonekana katika moja ya ligi tano bora Ulaya kama mambo yataenda kama tunavyotarajia. Kwa sasa tunasubiri majibu baada ya majaribio kukamilika."