Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaze aanza kibabe Ligi Kuu, Kagera Sugar ikiizima Mbeya City Sokoine

Muktasari:

  • Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Cedrick Kaze tangu atue kikosini akichukua mikoba ya Juma Kaseja aliyetemwa kutokana na matokeo ya kutoridhisha.

Mbeya;Baada kusota kwa muda mrefu hatimaye Kagera Sugar imeamka usingizini ikiikamua Mbeya City kwa mabao 3-1 na kufufua matumaini mapya Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Cedrick Kaze tangu atue kikosini akichukua mikoba ya Juma Kaseja aliyetemwa kutokana na matokeo ya kutoridhisha.

Kabla ya ushindi wa leo Oktoba 9 dhidi ya Mbeya City, Kagera Sugar ilicheza mechi sita mfululizo ikiambulia sare mbili na kupoteza nne na kuwa mkiani kwa pointi mbili.

Katika mchezo huo, Kagera Sugar ilitawala zaidi mpira na kufanya mashambulizi kadhaa japokuwa hazikuwa na usahihi kwa kuzuiwa na wapinzani.

Dakika ya 40, Emanuel Mvuyekule ndiye aliitanguliza Kagera Sugar kabla ya wenyeji Mbeya City kusawazisha kupitia kwa Hassan Hajji 'Cheda' dakika ya 44 na kwenda mapumziko wakiwa nguvu sawa.

Kipindi cha pili Mbeya City walipigiana pasi za hapa na pale, lakini ukuta wa Kagera Sugar ulikuwa imara kuharibu mipango huku wakitumia akili kutengeneza mashambulizi.

Dakika ya 53, Mudathir Said akipokea pasi ya Dickson Mhilu, alikunjuka shuti kali nje ya hatari na kuujaza mpira wavuni, akimuacha kipa wa City, Toba Kutusha asijue la kufanya.

Bao hilo lilionyesha kuongeza nguvu na ari kikosini ambapo dakika ya 79 Said tena aliingia kambani akiipatia bao la tatu Kagera Sugar na kuwachanganya wapinzani wao.

Matokeo hayo ni mwendelezo wa rekodi kwa Kagera Sugar kuutawala uwanja wa Sokoine ikiwa ni ushindi na muda mwingine sare.

Mbeya City inapoteza mechi ya pili nyumbani baada ya ile ya ufunguzi wa ligi dhidi ya Geita Gold 0-1, na kipigo cha tatu kwenye michuano hiyo ikiwamo dhidi ya Polisi Tanzania.

Ushindi wa 'Wanankurukumbi' hao unawanasua mkiani na kuchumpa hadi nafasi ya 14 kwa pointi tano huku City wakibaki nafasi yao ya sita kwa pointi 10 baada ya timu zote kucheza mechi saba.