Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kambi Yanga Dar kiboko

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Dar es Salaam. Yanga ina kila sababu ya kutikisa katika Ligi Kuu Tanzania Bara lakini pia hata upande wa Ligi Kuu ya Wanawake ambako kote inaongoza misimamo ya ligi hizo.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Mazingira ya kambi ya timu hizo mbili huko Kigamboni, Dar es Salaam yanatoa jibu la siri ya mafanikio ambayo timu ya wakubwa ya wanaume ya Yanga na ya wanawake, Yanga Princess zinayapata katika mashindano ambayo zinashiriki.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Katika ziara ya waandishi wa habari za michezo iliyofanyika kambini hapo jana, Mwananchi limebaini mambo kadhaa kuhusu kambi hiyo ambayo sio rahisi kuwepo kwa timu nyingine.

Kambi hiyo ipo katika mji wa kisasa wa Avic uliopo Somangira, Kigamboni umbali wa takriban kilomita 30 kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam, ina kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya maandalizi ya timu kuwa na ushiriki mzuri katika mashindano.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Ikiwa na nyumba za kisasa ambazo ndani zina huduma zote muhimu ambazo ni maji, umeme na luninga, kambi hiyo pia ina miundombinu inayoleta ufanisi kwa benchi la ufundi kutekeleza programu ambazo ni uwanja wa kisasa wenye nyasi za asili ambazo zinatunzwa vizuri pamoja na mabwawa ya kisasa ya kuogelea ambayo yanatumiwa na wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi kupoza miili pindi wanapomaliza programu za mazoezi.

Lakini pia pembezoni mwa uwanja wa soka upo mwingine wa mchezo wa mpira wa kikapu ambao pia unaweza kutumika kwa programu za kuongeza uimara wa kuruka, uharaka na ufiti wa mwili.

Moja ya mambo ya kushangaza katika kambi hiyo ni ulinzi ambao umewekwa ukifanywa na makundi mawili ambapo kundi la kwanza ni kampuni maalumu ya ulinzi yenye askari waliosambaa katika kila kona ya kambi ili kuhakikisha usalama hautetereki.

Ukiondoa kundi hilo, lingine ni lile la walinzi maalumu wa Yanga ambao hawakauki kambini na wamekuwa hawaruhusu mtu asiyefahamika au ambaye hana kibali maalumu kuingia katika eneo hilo linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa eka nne.

Na katika kuhakikisha usalama wa timu unazingatiwa hata ndani ya kambi hiyo, imekuwa ni nadra kwa wachezaji kuonekana nje pindi wanapokuwa hawana programu za mazoezi na muda mwingi hujifungia ndani katika majengo yaliyopo hapo.

Utaratibu wa programu za mazoezi katika eneo hilo huanzia kwa timu ya wanawake ya Yanga Princess na kisha wanafuatiwa na vijana chini ya umri wa miaka 20 na mwishoni huwa yale ya kikosi cha wakubwa.

Katika kile kinachoonekana kuwaondolea usumbufu wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi pindi wanapomaliza programu za mazoezi, mabwawa ya kuogelea, uwanja wa mazoezi pamoja na ukumbi wa chakula, vimewekwa jirani na hivyo kufanya kuwepo kwa urahisi wa kutoka eneo moja kwenda lingine.

Akizungumzia kambi hiyo, mshauri mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa alisema ni mahali panapohitajika kwa timu ya kisasa kupatumia.

“Nadhani ndugu waandishi leo mtapata fursa ya kujionea namna kambi yetu ilivyo na miundombinu yake kwa ajili ya kujenga timu bora na yenye ushindani,” alisema Mazingisa.

“Haya ni matokeo ya juhudi na ushirikiano wa pamoja na ndio maana hii inaitwa klabu na sio utashi wa mtu mmojammoja.”

Katika ziara hiyo ya jana, kundi kubwa la viongozi wa Yanga lilikuwepo kambini hapo likiongozwa na mwenyekiti Dk Mshindo Msolla, waandishi na baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo.