Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yakutana na wanahabari

Klabu ya Yanga leo inakutana na waandishi wa habari za michezo katika kambi ya timu hiyo iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo, waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari watapata fursa ya kufanya mahojiano ya moja kwa moja na viongozi, wadhamini, wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo.

Tukio hilo ambalo ni la kwanza kufanywa na klabu ya Yanga, litaongozwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Dk. Mshindo Msolla akiambatana na Makamu Mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela.

Kampuni zinazoidhamini Yanga ambazo ni GSM, Sportpesa, Maji ya Afya, Azam Media nazo zimetuma wawakilishi wao katika tukio hilo ambalo linafanyika katika kambi ya timu hiyo iliyopo Avic Town Kigamboni.

Tukio hilo limeanza saa 3.00 asubuhi na linatarajiwa kufanyika kwa siku nzima hadi saa 12 jioni.

Yanga imekuwa ikitumia kambi ya Avic Town, Kigamboni tangu mwaka 2019 ilipoingia mkataba wa udhamini na Kampuni tanzu ya GSM ambayo inahusika na gharama zote za kambi hiyo