Senzo: Hizi ndio sababu za Yanga Media Day

Mshauri wa uongozi wa Yanga, Senzo Mazingisa ametaja sababu tatu za klabu yao kuandaa siku maalum ya vyombo vya habari katika kambi yao.
Senzo amesema sababu ya kwanza ni kutoa fursa kwa wanahabari kujua na kuzungumza mambo ma mahusiano kati ya klabu yao na wadhamini wao.
"Siku zote Yanga ikicheza nafasi ya kuzungumza huwa kwa makocha, wachezaji wanafanya vizuri na kama ukiwa na bahati utaongea na nahodha.
"Leo ni tofauti nawaona wawakilishi wa wadhamini wetu Sportpesa, GSM, Afya, Taifa Gas muwaulize leo kwanini wanaidhamini Yanga na kuendelea kuwapa pesa.
Senzo amesema sababu ya pili ni kutoa nafasi kwa waandishi kujua mazingira ya kambi yao iliyopo Kigamboni na kujua mazingira yake.

Amesema sababu ya tatu ni kutoa nafasi kwa wanahabari kujua taarifa za wachezaji wote wa timu yao.
"Inawezekana wapo ambao hawakuwa hawapati nafasi ya kuwapata wachezaji wetu na kujua mambo mbalimbali na hii ni nafasi muhimu kwenu.
Aidha Senzo amesema hatua nyingine muhimu ya kuwa na siku hii itawasaidia wanahabari kujua maendeleo ya mchakato wao wa mabadiliko.
"Mtauliza maswali juu ya maendeleo ya mabadiliko ya mfumo wetu wa uendeshaji klabu imefikia wapi hapa leo kuna viongozi wote wa muhimu mtauliza maswali yenu na mtapata majibu yote,"