Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kakolanya awapa tahadhari makipa Kariakoo Dabi

KAKOLANYA Pict

Muktasari:

  • Kakolanya ambaye ni kipa wa zamani wa Simba na Yanga amesema Kassali ambaye alizaliwa Julai 5, 1996 nchini Niger licha ya kuzidiwa uzoefu wa dabi na Diarra, haiondoi wawili hao kukwepa changamoto ya kufikiwa  mara kwa mara na washambuliaji wa timu hizo, huku akitarajia itakuwa mechi nzuri na ya ushindani.

KIPA wa zamani wa Simba na Yanga, Beno Kakolanya ambaye kwa sasa anaichezea Polisi Tanzania, ameizungumzia Kariakoo Dabi na tahadhari kwa makipa Djigui Diarra wa Yanga na Djibrilla Kassali wa Simba kujipanga kukabiliana na washambuliaji wa timu hizo.

Kakolanya ambaye ni kipa wa zamani wa Simba na Yanga amesema Kassali ambaye alizaliwa Julai 5, 1996 nchini Niger licha ya kuzidiwa uzoefu wa dabi na Diarra, haiondoi wawili hao kukwepa changamoto ya kufikiwa  mara kwa mara na washambuliaji wa timu hizo, huku akitarajia itakuwa mechi nzuri na ya ushindani.

“Nikiangalia Simba ina wachezaji kama Clatous Chama, Libasse Gueye vivyo hivyo kwa Yanga kuna Max Nzengeli, Peter Shalulile, hizo timu zina wachezaji wazuri, lazima makipa watakutana na chalenji kubwa ni wao kuongeza umakini wa namna ya kuwakabili na kuzungumza mara kwa mara na mabeki wao kuona hatari kabla hawajafikiwa,” amesema.

KAKO 01

Data za mastaa hao, Gueye ni kinara wa asisti tano, bao moja, Chama mabao manne, Nzengeli mabao matatu, asisti moja, Shalulile mabao matatu, asisti moja, Ki asisti moja. Utofauti wa uzoefu wao katika dabi kwa Kassali aliyejiunga na Simba msimu wa 2025/26 akitokea AS FAN hiyo itakuwa ya msimu wake wa pili, lakini kwa Diarra itakuwa dabi yake ya sita tangu alipojiunga na Yanga 2021/22 hadi 2026/2027.

“Dabi haina mazoea nimecheza timu zote mbili, naelewa ugumu wake ndiyo maana nimezungumzia nafasi ninayocheza kwamba wote wawili watakabiliwa na kukutana mara kwa mara na washambuliaji pamoja na mabeki wa pembeni,” amesema.