Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kabunda, Mfuko wajisogeza Mashujaa

KABUNDA Pict

Muktasari:

  • Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kumalizana na timu hiyo ni kiungo mshambuliaji Hassan Kabunda na beki wa kati, Abdallah Mfuko wote kutoka Namungo. 

TIMU ya Mashujaa iliyomaliza msimu wa 2025-2026 ikiwa nafasi ya 11 na pointi 33 katika Ligi Kuu Bara, imeanza kukifanyia marekebisho kikosi chake huku tetesi zikidai kuwa timu hiyo inasajili wachezaji watakaongeza nguvu ya ushindani kwa msimu ujao.

Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kumalizana na timu hiyo ni kiungo mshambuliaji Hassan Kabunda na beki wa kati, Abdallah Mfuko wote kutoka Namungo.

Watu wa karibu na wachezaji hao wamesema tayari timu ya Mashujaa imemalizana nao, hivyo ni suala la muda kutambulishwa kwa mashabiki wa timu hiyo.

KABU 02

“Kila kitu kimekamilika, imebakia tu kwa viongozi kuwatangaza mbele ya mashabiki wao, uzoefu wao wameona utaisaidia timu hiyo kumaliza nafasi za juu zaidi kwenye msimamo wa ligi tofauti na uliyopita,” kimesema chanzo hicho.

KABU 01

Alipotafutwa Mfuko amesema: “Siwezi kuzungumzia chochote kuhusiana na usajili wa nitacheza wapi, itafika muda sahihi kila mtu atajua nitakuwa na timu gani.”

Alipotafutwa meneja wa Mashujaa, Athuman Athuman ili kuthibitisha hilo amesema: “Nipo kijijini kwetu siwezi kujua ishu za usajili kwa sasa, hivyo sina cha kukwambia kuhusiana na jambo hilo nikiwa nje ya kazi labda nikisharudi kuungana na timu nitakwambia.”