Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Joti, Gigy Money waula ubalozi WinPrincess

Wasanii Gift Stanford 'Gigy Money' na Lucas Mhuvile 'Joti' wamepewa ubalozi wa mchezo wa  kubashiri wa WinPrincess.
Wawili hao walitangazwa kuwa mabalozi na Meneja  wa WinPrincess, Hakan Aric.

Aric amesema wamewachagua wasanii hao kutokana na kuwa na  wafuasi wengi ambapo wanaamini kupitia wao wataweza kuwashawishi watu kucheza mchezo huo kupitia WinPrincess.

"Wasanii wapo wengi, lakini kwetu sisi Gigy na Joti tumeona watatusaidia kufikisha ujumbe kwa wateja wetu," amesema.

Kwa upande wake Gigy Money aliahidi kutumia umaarufu alionao kuitangaza kampuni hiyo ili kuwaongezea wateja.

Wakati  meneja wa Joti, Peter Mkoba aliyekuwa anamwakilisha msanii huyo katika hafla hiyo, alishukuru kwa kumuona msanii wake na kuahidi kuwa hawatamuangusha.

Naye Meneja Masoko wa Tele-Marketing kutoka WinPrincess Sports Betting, Winny Macha alisema; "Sisi kama WinPrincess tunaamini katika uaminifu na tuko hapa kutoa imani kwa wateja wetu kwa kutangaza Kauli mbiu yetu,"

"Ushindi ni Papo Hapo" ambayo ina maana mshindi ana uhakika wa Malipo ya Papo Hapo kutokana na ushindi,