Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Job aanza na majukumu mapya

JOB Pict

Muktasari:

  • Job alirejea uwanjani Oktoba 21, 2026, akiingia dakika ya 68 na kuchukua nafasi ya nahodha Bakari Mwamnyeto, katika mchezo ambao Yanga iliichapa CFFA ya Madagascar mabao 4-1, na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

BAADA ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani siku 234 kutokana na jeraha la goti, beki wa Yanga, Dickson Job, amerejea rasmi uwanjani juzi wakati Yanga ilipoiondosha CFFA ya Madagascar kwa jumla ya mabao 8-1 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akicheza nafasi mbili uwanjani.

Job alirejea uwanjani Oktoba 21, 2026, akiingia dakika ya 68 na kuchukua nafasi ya nahodha Bakari Mwamnyeto, katika mchezo ambao Yanga iliichapa CFFA ya Madagascar mabao 4-1, na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Beki huyo aliumia Machi 1, 2026, katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba, uliopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Jeraha hilo lilimlazimu kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini Machi 11, 2026.

Hata hivyo, kurejea kwake hakukuwa tu suala la kurudi uwanjani, bali pia kukubali majukumu mapya ndani ya timu. Katika mchezo dhidi ya CFFA, Job alianza kutumika kama beki wa kati kabla ya baadaye kuhamishiwa nafasi ya kiungo mkabaji mkabaji baada ya kuchukua nafasi ya Fred Ngoma.

JO 01

Akizungumzia kurejea kwake, Job amesema alifurahi kupata nafasi ya kucheza tena, huku akiwashukuru Watanzania, uongozi wa timu, benchi la ufundi, wachezaji wenzake na familia yake kwa sapoti waliyompa wakati wote alipokuwa nje.

Kuhusu kupewa majukumu mawili tofauti katika mchezo huo, Job amesema kocha alimweleza mapema mpango wa kumtumia katika nafasi hizo, hivyo alikuwa tayari anafahamu.

JO 02

“Kocha aliniambia kabla ya mchezo kuwa ningeingia kucheza kama beki wa kati, kisha baadaye Ngoma akitolewa ningeenda kucheza namba sita,” amesema Job, akifafanua namna alivyopangiwa majukumu yake.

“Nilipokea maelekezo haya kwa sababu nilikuwa nimeshafanya mazoezi ya kutosha na nilikuwa tayari kutekeleza kile ambacho benchi la ufundi linahitaji kutoka kwangu.”