Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jabiri :Nimeanza na upepo mzuri

Muktasari:

  • Hadi sasa Jabiri, amefunga mabao matano na asisti moja baada ya kucheza mechi sita za ligi, jambo ambalo alisema kwake ni hatua kubwa anatamani hadi mwisho wa msimu amalize na mabao zaidi ya 10, ili awe katika tano bora ya washambuliaji waliofanya vizuri.

MSHAMBULIAJI wa Polisi Tanzania, Anuary Jabiri amesema amekuwa na mwanzo mzuri wa kufunga mabao, jambo linalompa taswira ya kuamini utakuwa msimu mzuri kwake na kufunga mabao mengi.

Hadi sasa Jabiri, amefunga mabao matano na asisti moja baada ya kucheza mechi sita za ligi, jambo ambalo alisema kwake ni hatua kubwa anatamani hadi mwisho wa msimu amalize na mabao zaidi ya 10, ili awe katika tano bora ya washambuliaji waliofanya vizuri.

Jabiri ambaye msimu uliopita haukuwa na bao hata moja alisema: “Simaanishi ni msimu mrahisi, lakini nina upepo wa kufunga, hivyo nazidisha bidii na mazoezi ili kuhakikisha nafikia ndoto zangu za msimu huu.

“Lakini malengo makuu ni kuhakikisha naisaidia timu kufikia malengo yake, timu inapofanya vizuri basi na wachezaji tunakuwa kwenye kiwango kizuri, kila kitu kikifanyika kwa umoja kinakuwa na mafanikio makubwa.”

Polisi Tanzania katika mechi sita ilizocheza, imeshinda tatu, sare moja, imefungwa mbili, mabao ya kufunga ni tisa yenyewe ikifungwa mara saba  kwa sasa ikiwa na pointi 10 ikiwa nafasi tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu.