Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Imekuwa Jumapili ngumu kwa Simba 

SIMBA Pict

Muktasari:

  • Asubuhi Simba ilifanya mkutano ambao ulimalizika kitatanishi baada ya Mwenyekiti, Murtaza Mangungu na kusababisha wanachama kumcharukia, lakini usiku huu katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya Stade Malien ilipoteza kwa mabao 2-1.

LICHA ya wenyewe kujinasibu kwamba Jumapili huwa ni siku nzuri kwa klabu yao, lakini hali kwa Jumapili ya leo imekuwa kinyumw kwa Simba baada ya awali kuvurugana katika Mkutano Mkuu wa mwaka mapema asubuhi na usiku huu imekumbana na kipigo cha pili ikiwa ugenini huko Mali.

Asubuhi Simba ilifanya mkutano ambao ulimalizika kitatanishi baada ya Mwenyekiti, Murtaza Mangungu na kusababisha wanachama kumcharukia, lakini usiku huu katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya Stade Malien ilipoteza kwa mabao 2-1.

Awali ikicheza nyumbani wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba ililala kwa bao 1-0 mbele ya Petro Atletico ya Angola inayoongoza msimamo kwa kubebwa na herufu kwani imelingana kila kitu na Malien kila moja ikiwa na pointi nne na mabao manne.

SIM 01

Wenyeji walikuwa na kipindi bora cha kwanza wakiishambulia Simba kwa nguvu walitengeneza nafasi nyingi za kutafuta mabao.

Alikuwa mshambuliaji Taddeus Nkeng aliyezitingisha nyavu za Simba akifunga bao safi kwa mguu wa kulia akimalizia pasi ya kichwa ya Moussa Diallo ikiwa ni dakika ya 16.

Wakati Simba inajiuliza italirudishaje bao hilo , ikaruhusu jingine bao la pili dakika ya 23 la kichwa mfungaji akiwa beki Ismaila Simpara akitumia mpira wa Kona ya Abdul Bode.

Simba ikipoteza nafasi nzuri kupitia Joshua Mutale shuti lake linapaa akipokea krosi ya Seleman Mwalimu na kufanya Wekundu waende mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 2-0.

SIM 02

Kipindi cha pili Simba ilirudi na mabadiliko matatu yaliyowabadilisha ikiwatoa Jean Charles Ahoua Mutale, Rushine de Reuck na Mwalimu nafasi zao zikichukuliwa na Chamou Karaboue Allasane Kante, Jonathan Sowah na Morris Abraham.
Mabadiliko hayo yaliwasaidia Simba na kusawazisha bao la kwanza likifungwa na Neo Maema kwa shuti Kali la nje ya eneo la hatari.

Kipa wa Simba Yakub Seleman aliiokoa timu yake isiruhusu bao la tatu baada ya kupangua mkwaju wa penalti dakika ya 76 iliyopigwa na Nkeng.

SIM 03


Simba ikapata pigo baada ya Kante kupewa kadi nyekundu ya Moja kwa Moja baada ya kumvuta mshambuliaji wa Malien.
Vikosi vilivyocheza;

STADE MALIEN: N'golo Traore,Abdul Bode,Francis Awine,Babe Diarra,Ismaila Simpara,Ahmadou Belo,Ibrahima Camara/Haman ,Mamadou Traore,Ousmane Koulibaly,Taddeus Nkeng,Moussa Diallo

SIMBA: Yakoub Seleman, Shomari Kapombe, Antony Mligo, Rushine de Reuck/Chamou Karaboue, Wilson Nangu, Naby Camara, Joshua Mutale/Morris Abraham, Jean Charles Ahoua/, Neo Maema,Seleman Mwalimu/Jonathan Sowah, Ellie Mpanzu