Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ibenge ampa mzuka Fei Toto

FEI TOTO Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo amezungumza hayo wakati kikosi cha Azam kikikabiliwa na mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya KMKM, itakayopigwa kesho Jumamosi Oktoba 18, 2025 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto', amesema kufundishwa na Kocha, Mkongomani, Florent Ibenge ni hatua kubwa kwa timu hiyo kufikia malengo iliyojiwekea hasa michuano ya kimataifa.

Nyota huyo amezungumza hayo wakati kikosi cha Azam kikikabiliwa na mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya KMKM, itakayopigwa kesho Jumamosi Oktoba 18, 2025 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

"Ni motisha kwetu kama wachezaji lakini ni changamo pia kubwa iliyokuwa mbele yetu kufikia na kutimiza malengo yetu ambayo tumeyadhamiria kuyafikia pamoja msimu huu," amesema Fei Toto.

FEI 01

Akiizungumzia KMKM, Fei Toto amesema anaamini itakuwa ni mechi ngumu kwa pande zote kutokana na miamba hiyo kujuana vyema kwani imeshakutana katika michuano mbalimbali.

"Tunaiheshimu KMKM kwa sababu ni timu nzuri lakini sisi kama wachezaji tumejipanga pia vizuri kuhakikisha tunatimiza azma ya kuingia hatua ya makundi, haitokuwa rahisi kwani zinapocheza timu za Bara na visiwani huwa ushindani unakuwa ni mkubwa," amesema.

FEI 02

KMKM imefika raundi ya pili ya michuano ya CAF baada ya kuitoa AS Port ya Djibouti kwa jumla ya mabao 4-2, huku kwa upande wa Azam ikiitoa EL Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini kwa jumla ya mabao 4-0.