Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hersi, Arafat wapitishwa Yanga kwa kishindo

URAIS Pict

Muktasari:

  • Hersi na Arafat ambao walikuwa wagombee pekee wa nafasi hizo, wamepitishwa na wanachama baada ya kuridhia kwa kauli moja kuendelea kuiongoza Yanga katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika leo Agosti 2, 2026, kwenye Ukumbi wa The Super Dome uliopo Masaki jijini, Dar es Salaam.

RAIS wa Yanga, Injiani Hersi Said na makamu wake, Arafat Haji, wamepata ridhaa kutoka kwa wanachama wa klabu hiyo kwa ajili ya kuongoza tena kwa miaka minne.

Hersi na Arafat ambao walikuwa wagombee pekee wa nafasi hizo, wamepitishwa na wanachama baada ya kuridhia kwa kauli moja kuendelea kuiongoza Yanga katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika leo Agosti 2, 2026, kwenye Ukumbi wa The Super Dome uliopo Masaki jijini, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Yanga, Malangwe Mchungahela, amesema baada ya Wanachama wa Yanga kuridhia kwa kauli moja, Hersi na Arafat wameshinda nafasi walizokuwa wanagombea kwa miaka minne.

"Kwa mujibu wa ibara ya 23 (3) na 24 (1), nawatangaza rasmi Hersi na Arafat kushika nyadhifa ya Urais na Makamu wa Urais," amesema Mchungahela.

Matokeo hayo yaliamsha shangwe kwa wanachama 877, waliohudhuria mkutano huo, huku wakiwa na furaha na matumaini makubwa kwa uongozi wa Hersi na Arafat kwa kipindi cha miaka minne ijayo, baada ya kufanya vizuri tangu walipoingia madarakani Julai 9, 2022.