Prime
Hatma ya Mayele Yanga iko hivi

Muktasari:
- Kikao hicho kilihusisha pia wasimamizi wa mchezaji huyo ambao wanapushi staa huyo akiwashe Arabuni ambako kuna mkwanja mnene na wako tayari kununua mkataba uliosalia Yanga
Licha ya kufanya siri kubwa, lakini tumejua kwamba vigogo wa Yanga juzi usiku walikuwa na kikao kizito na Fiston Mayele nyumbani kwake Mbezi Beach karibu na ufukwe wa Bahari ya Hindi.
Mayele mwenye mkataba wa mwaka mmoja na Yanga amegoma kusaini mkataba mpya ambao ungemfanya awe analipwa pesa ndefu kuliko mchezaji yeyote ndani ya timu hiyo huku akidaiwa amepagawa na ofa nono kutoka Esperance ya Tunisia, Zamalek, Pyramids za Misri, timu za ubelgiji na Qatar.
Kikao hicho kilihusisha pia wasimamizi wa mchezaji huyo ambao wanapushi staa huyo akiwashe Arabuni ambako kuna mkwanja mnene na wako tayari kununua mkataba uliosalia Yanga
Bado hawajafikia muafaka wa kusalia au kuondoka ingawa tajiri ahidi dau nono lakini juzi mchana alionekana kwenye sehemu Jijini Dar es Salaam akipiga picha za matangazo ya uzi mpya wa Jangwani ambao umetangazwa jana usiku nchini Malawi.
Mshambuliaji huyo kupiga picha na uzi wa Yanga kwa ajili ya tangazo ni jambo ambalo linaashiria lolote linaweza kutokea.