Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hall aishambulia Taifa Stars

Kacha wa timu ya Zanzibar Heroes na Aam Fc,Stewart Hall

Mwandishi Wetu KOCHA wa timu ya Azam FC, Stewart Hall amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, kuachana na utaratibu wa kucheza kamari kwa kuajiri makocha kwa mikataba ya muda mfupi kisha wakatarajia kupata mafanikio makubwa. Alisema mafanikio ya soka yanakuja kwa njia ya maandalizi ya muda mrefu lakini si kwa kuajiri kocha kwa miaka miwili huku akipewa timu isiyokuwa na malengo. Kocha huyo raia wa England, alisema kuwa kamwe soka ya Tanzania haiwezi kupiga hatua kwa sababu ya programu za TFF zinakosa malengo endelevu. Kwa aina ya soka la Tanzania na aina ya wachezaji waliopo mafanikio ya soka hayawezi kupatikana bila ya kuweka mikakati ya muda mrefu, huwezi kumwajiri kocha kwa mkataba wa miaka miwili kisha ukatarajia mafanikio,alisema Hall. Alisema soka ya Tanzania inahitaji mikakati ya muda mrefu ikiwa ni sanjari na kuboresha ligi, kuandaa vituo vingi vya kukuza vipaji huku TFF pia ikitakiwa kuandaa timu nne za taifa za vijana kuanzia umri wa miaka 15, 17, 20 na 23 ambazo zinatambulika wakati wote sio zile za kuandaliwa wakati wa mashindano tu. Akifafanua zaidi juu ya mikataba ya makocha hapa nchini Hall, alisema TFF wanapaswa kuajiri kocha wa timu ya taifa ya wakubwa kwa miaka mitano huku timu za vijana pia zikiwa na makocha wa muda mrefu ambao wanaweza kuwa wazawa ama wageni. Kitendo cha kumwajiri kocha kwa miaka miwili kisha unampa timu ambayo inahitaji kufundishwa soka upya kuanzia kutuliza mpira, kupiga chenga, kumiliki mpira, kupiga krosi, kupiga kona, kumtoka adui, na kufunga magoli ndani ya miaka miwili ni kujidanganya. Hakuna kocha wa timu ya Taifa mwenye uwezo wa kufanya mambo hayo yote duniani kwa kipindi cha miaka miwili, inatakiwa kocha aje kuunganisha mfumo, lakini kwa Tanzania unaanza a, e, i, o, u, alisema Hall. Alisema hayo mambo hayawezekani kwa sababu kocha wa timu ya taifa anakutana na wachezaji kwa kipidi kisichozidi wiki mbili tu kwa sababu wachezaji hao wanakuwa katika klabu zao muda wote. Alifafanua kuwa ili Tanzania ipige hatua katika soka wazingatia ubora wa ligi na aina ya wachezaji wanaosajiliwa kucheza ligi hiyo huku wakimwajiri kocha kwa muda mrefu kisha wamkabidhi timu ya vijana ya U-20 kwa muda wa miaka mitano. Akizungumzia uwezo wa wachezaji walioko katika timu ya taifa, Taifa Stars kwa sasa alisema ni wachezaji wazuri lakini wengi wana umri mkubwa na viwango vyao vimeanza kushuka hivyo si wachezaji wanaotarajiwa kuleta mafanikio katika mechi za kimataifa hasa mbele ya mataifa yenye malengo ya mbali katika soka. Akitolea mfano wa wachezaji tegemeo katika timu hiyo alisema ni Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaocheza soka TP Mazembe kuwa wana umri mdogo kiasi kwamba kuwategemea wao peke yao ni kuwapa mzigo mkubwa na pengine hali hiyo inawafanya washindwe kucheza vizuri kwa sababu ya umri wao. Akitumia mfano hali katika maisha ya jamii, alisema kuwa, mtoto mwenye umri mdogo anapopewa mzigo mkubwa aubebe nikumuumiza hivyo anaweza kuufikisha unapotakiwa ufike ama safasi yake ikaishia njiani na kwamba huo ni sawa kucheza kamali. Soka sio mchezo wa kamari soka ni sawa na maisha kwa sababu maisha kadri ulivyojiandaa ndivyo unavyofanikiwa ukifanya maandalizi mabaya kuanzia utotoni nikimaanisha kuanzia elimu yako huwezi kufanikiwa uzeeni, alisema Hall ambaye ana jukumu la kuinoa Zanzibar Heroes katika michuano ya Chalenji inayoanza Ijumaa ijayo.