Gomes amtengeneza Ajibu mpya

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

SIMBA imecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara bila mshambuliaji wao Ibrahim Ajibu ambaye kwasasa ameanza kuonyesha kiwango bora mazoezini na kumshawisho kocha wake Didier Gomes aliyetamka kuwa huenda akaanza kumtumia mechi zijazo.

SIMBA imecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara bila mshambuliaji wao Ibrahim Ajibu ambaye kwasasa ameanza kuonyesha kiwango bora mazoezini na kumshawisho kocha wake Didier Gomes aliyetamka kuwa huenda akaanza kumtumia mechi zijazo.

Katika mazoezi yao yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterani, Ajibu alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliojituma kwa kila mazoezi aliyofundisha kocha wao.

Kwa mara ya mwisho, Ajibu kucheza mechi ya mashindano ya timu yake ni msimu uliopita walipokutana na Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa Mkapa akitokea benchi kuchukuwa nafasi ya Bernard Morrison.

Katika nafasi yake, Gomes ameongeza nyota wawili wapya Kibu Denis na Ousmane Sakho.

Gomes ameliambia Mwanaspoti kuwa; “Namuona Ajibu mpya kutokana na vita kubwa na juhudi anazozionyesha mazoezini na amekua na maendeleo mazuri hasa upande wa kuboresha uimara, ameongeza umahiri wa kufunga na kulenga mashuti langoni pia ameanza kuingia kwenye falsafa zangu”

“Pia ameongeza kiwango cha nidhamu pongezi kwa hilo kitu ambacho nimekua nikikisisitiza mara nyingi kambini, msimu huu nitafurahi kuona kila mchezaji akipata nafasi ndani ya kikosi hivyo basi natarajia kumuona Ajibu kurudi tena kwenye kikosi kuleta ushindani pamoja na kuisaidia Simba kupata matakeo mazuri mechi zijazo,” alisema Gomes.