Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

GEORGE MASATU: Gulamali aligushi saini yangu na Hussein Marsha -1

Muktasari:

Beki mkongwe wa timu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, George Magere Masatu ni miongoni mwa wachezaji waliopata sifa kubwa katika mchezo wa soka hapa nchini lakini kwa hivi sasa jina lake halisikiki tena.

KATIKA maisha kuna mambo yanayoweza kukupandisha ama kukushusha, ndivyo ilivyo hasa kwa wachezaji, wanamuziki na waigizaji wa filamu na wengine wenye fani kama hizo.

Mtu anaweza kutamba na kusifika katika jamii lakini mambo yakimuendea kombo anapotea na jina lake kufutika katika jamii.

Beki mkongwe wa timu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, George Magere Masatu ni miongoni mwa wachezaji waliopata sifa kubwa katika mchezo wa soka hapa nchini lakini kwa hivi sasa jina lake halisikiki tena.

Pamoja na kwamba hasikiki tena lakini linapotajwa jina lake lazima utakumbuka mambo mengi kuhusu mchezaji huyo aliyeibuliwa na Pamba FC ya jijini Mwanza.

Masatu ambaye kwa sasa makazi yake yapo jijini Dar es Salaam akiishi pamoja na ndugu zake alifanya mahojiano maalumu na Mwanaspoti na kuelezea mambo mbalimbali ya soka ndani na nje ya nchi pamoja na maisha yake binafsi kwa jumla.

Safari ya kwenda Simba

Masatu alikuwa ni rafiki mkubwa ambaye alikuwa pia ni mchezaji mwenzake, Hussein Amani Marsha.

Mchezaji huyo alikuwa ni kama pacha wake kwa kuwa walikuwa karibu na walifanya uamuzi wa kutoka Pamba pamoja na kuhamia katika Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam.

Ilikuwa watue Yanga

Kabla ya kutua katika timu hiyo, yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam mwaka 1991, Masatu na Marsha walikuwa watue kwa mahasimu wa Simba yaani Yanga.

“Tuliachana na mkataba wa Yanga ambao tulishaanza nao mazungumzo na kusajili Simba,”anasema Masatu na kuongeza kwamba viongozi wa Yanga hawakuwa wakieleweka ingawaje walishasaini fomu mama na kubakiza za uhamisho kutoka Pamba.

Ilikuwaje?

Masatu anasema kuwa wakati huo, Yanga ilikuwa chini ya Abbas Gulamali ambaye alikuwa akifanya mazungumzo nao lakini ilifikia hatua Masatu na Marsha walishtuka na kubadilisha mwelekeo.

“Tuliahidiwa kupewa Sh 1.5 milioni kila mmoja lakini Gulamali alitupa Sh. 750,000 kila mmoja kama nusu ya fedha tuliyokubaliana huku akituahidi kutumalizia baada ya kukamilisha uhamisho wetu baada ya wiki moja lakini hakufanya hivyo.

Saini zao ziligushiwa

Masatu anasema kuwa walihisi kulikuwa na ujanja katika usajili wao wa kwenda Yanga na hivyo waliongeza umakini ili wasiingizwe mjini.

“ Gulamali alitaka kutufanyia usanii ambapo aligushi saini zetu na kudai kwamba ametusainisha na fomu za uhamisho jambo ambalo tulilishtukia mapema na kuwamabia viongozi wetu wa Pamba wazuie na wasiwape fomu hizo mpaka pale sisi tutakapokuwepo ili tuweke mambo wazi,” anasema na kuongeza

Nani aliyewashawishi kwenda Yanga?

Kiungo wa Yanga Athuman Abdallah China ndiye aliyewashawishi Masatu na Marsha kujiunga na Yanga kila walipokuna naye.

“Ilifikia hatua China aligombana na Gulamani kwa kushindwa kumalizana nasi, hapo mawazo yetu yalibadilika kwani tuliona haikuwa vyema tena kuendelea na mipango ya kujiunga na Yanga.”

Watua Msimbazi

Duniani hakuna siri, baada ya mfadhili wa Simba wa wakati huo, Azam Dewji kusikiwa kwamba Gulamali ameshindwa na wachezaji hao akaamua kuwatafuta.

“Dewji alituita na tukafanya naye mazungumzo, wakati huo tukiwa timu ya Taifa, Dewji alituahidi kutupa Sh.3 milioni, tulikubali na tulirudisha fedha za Gulamali kwani tulikuwa bado hatujaitumia.

“Dewji alitukatia tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi Mwanza ili tukalipwe fedah zetu, tuliomba ruhusa kwa kocha wa timu ya taifa wakati huo alikuwa Zacharia Kinanda na huo ukawa mwanzo wa sisi kuichezea Simba,” anasema Masatu.

Tuhuma Taifa Stars

Katika vitu ambavyo, Masatu hawezi kuvisahau katika maisha yake ni yeye pamoja na pacha wake, Masha kutuhumiwa kuzihujumu timu za Simba na Taifa Stars.

Anasema kwamba wakiwa na Simba, waliwahi kutumiwa kucheza chini ya kiwango katika michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali.

“Ni kweli tulituhumiwa lakini hakikuwa kitu cha kweli, mambo kama hayo huwa yanatokea sana katika soka hasa timu zinapofanya vibaya, lakini pia nilituhumiwa katika timu ya Taifa kuwa nilijifanya nimeumia il nischeze mechi na nije kucheza mechi ya Simba na Yanga na ilidaiwa Dewji ndiye aliyenishawishi nijifanye nimeumia.

“Ukweli ni kwamba, niliumia wakati nakiokoa goli wakati Stars ikicheza na Ivory Coasta, kipa Steven Nemes, alitoka golini, hivyo ilikuwa ni lazima nikimbie na kwenda kuokoa goli na kujikuta mguu wangu ukijigonga kwenye mwamba wa goli na kuumia mguu wangu wa kulia.

“Nilisikia maumivu kwa ndani, jambo ambalo lilisabisha mguu kuvimba taratibu na mtu mwingine haikuwa rahisi kugundua kama nimeumia,” anasema.

Ilikuwaje?

Beki huyo mfupi aliyeweza kumudu vyema kucheza namba tano anasema kwamba utata wa tuhuma hizo ulianzia katika mechi ya Ghana iliyochezwa jijini Mwanza.

“Nilikwenda na kulazimishwa kucheza na viongozi wa Fat lakini nilishindwa kabisa na kuwaambia ukweli kuwa siwezi kucheza nina maumivu makali, hapo ilibaki siku chache mechi ya Simba na Yanga ichezwe, kweli sikucheza na walikasirika sana na kunituhumu moja kwa moja bila kificho,” anasema.

“Usiku maumivu yalikuwa makali mno, nilimwita daktari wa timu, Dk. Seleman ambaye aliniambia tatizo langu ni kubwa hivyo nikapelekwa hospitali ya Aghakan ambako pia walisema kesi yangu ni kubwa niende Muhimbili, lakini cha ajabu nilibaki Mwanza bila kupata hudumu yoyote kutoka Fat kwa wakati huo.

“Hiyo ni kwa sababu waliamini kwamba nilikuwa na mpango wa kuihujumu timu pamoja na Dewji ili nicheze mechi ya Simba na Yanga, matokeo katika mechi hiyo na Ghana ilikuwa ni sare ya mabao 2-2,” anasema.

Mganga wa kienyeji

Kutokana na maumivu hayo kumsumbua kwa muda mrefu baadhi ya ndugu wa Masatu walitaka kumpeleka mchezaji huyo wa waganga wa kienyeji katika Visiwa vya Ukerewe.

“Walitaka kunipeleka kwa wataalumu lakini niliwasiliana na Dewji na kumweleza majibu ya hospitali hivyo alinitumia tiketi ya ndege na kuniambia nirudi Dar es Salaam haraka ili niende Muhimbili kwa matitabu zaidi, hivyo safari ya Ukerewe ikafa.

Makala hii itaendelea Jumanne ijayo ambapo Masatu ataendelea kufunguka vitu vingine vingi zaidi.