Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geita Gold kuamua leo kupanda Ligi Kuu Bara

Muktasari:

  • Geita inayofundishwa na Kocha, Zubery Katwila ilishuka daraja msimu wa 2023-2024, ambapo ushindi wa leo dhidi ya timu ya Songea United kwenye Uwanja wa Nyankumbu mjini, Geita, utaifanya kurejea Ligi Kuu Bara, kwani itafikisha pointi zake 71.

HISTORIA mpya inaenda kuandikwa leo kwenye Uwanja wa Nyankumbu mjini, Geita, wakati Geita Gold ikisaka ushindi wake wowote dhidi ya Songea United ili kupata tiketi ya kurejea Ligi Kuu Bara.

Geita inayofundishwa na Kocha, Zubery Katwila ilishuka daraja msimu wa 2023-2024, ambapo ushindi wa leo dhidi ya timu ya Songea United kwenye Uwanja wa Nyankumbu mjini, Geita, utaifanya kurejea Ligi Kuu Bara, kwani itafikisha pointi zake 71.

Iko hivi, Geita vinara ikiwa na pointi 68, baada ya kushinda mechi 21, sare tano na kupoteza moja kati ya 27, japo ikiwa itaifunga Songea United itafikisha 71, ambazo zitaihakikishia kupanda rasmi daraja na kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

Kwa maana hiyo Geita Gold ikishinda itafikisha pointi 71, ambazo haziwezi kufikiwa na Polisi Tanzania inayoshika nafasi ya tatu na pointi 60, kwani ikishinda mechi zote tatu itaishia 69, kwa sababu zinazopanda moja kwa moja ni timu mbili.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Mkuu wa Geita Gold, Zubery Katwila alisema licha ya kutambua umuhimu wa mechi hiyo, ila amewataka wachezaji wa kikosi hicho kucheza kwa tahadhari na kuepuka presha inayoweza kuwaharibia siku yao.

Mechi nyingine zitakazopigwa leo, Kagera Sugar itakuwa kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba kuikaribisha KenGold ya Mbeya.

Kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi, Bigman FC baada ya kutoka sare ya bao 1-1, dhidi ya Stand United, itaikaribisha Gunners FC ya jijini Dodoma, yenye morali kubwa kutokana na wiki iliyopita kuishangaza Mbeya Kwanza ugenini kwa kuichapa mabao 2-1.

Mbeya Kwanza baada ya wiki iliyopita kushindwa kutamba na kuchapwa mabao 2-1, dhidi ya Gunners FC, itakuwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora, ikiikaribisha Stand United ‘Chama la Wana’, iliyotoka sare ya bao 1-1 na Bigman FC.

Kwenye Uwanja wa Amani mjini Njombe, Hausung FC inayoburuza mkiani mwa msimamo mwa nafasi ya 16 na pointi tisa, baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1, dhidi ya Barberian, itaikaribisha Transit Camp iliyotoka suluhu (0-0) mbele ya B19 FC.

Barberian FC iliyo nafasi ya 15 na pointi 12, baada ya sare ya bao 1-1, dhidi ya Hausung FC, itaikaribisha B19 FC kwenye Uwanja wa Filbert Bayi mkoani Pwani, huku Mbuni ikiwa mwenyeji kwa kukikaribisha kikosi cha maafande wa Polisi Tanzania.

Mbuni inaingia katika mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu nzuri baada ya wiki iliyopita kuifunga African Sports ya Tanga bao 1-0, sawa na wapinzani wao Polisi Tanzania inayoshika nafasi ya tatu na pointi 60, iliyoifunga TMA ya Arusha mabao 2-0.

Mechi nyingine ya kuhitimisha raundi ya 28, itapigwa kwenye Uwanja wa Black Rhino jijini, Arusha, ambapo TMA FC iliyochapwa mabao 2-0, na Polisi Tanzania, itacheza dhidi ya African Sports, iliyofungwa bao 1-0 na Mbuni FC.