Francis Kifukwe wa Yanga, afariki dunia akipatiwa matibabu India
Muktasari:
- Kifukwe amefariki jana saa 3 usiku kwa muda wa Tanzania, akiwa nchini humo ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Rais na Mjumbe wa zamani wa Baraza la Wadhamini la Yanga, Francis Kifukwe amefariki dunia jana Ijumaa Agosti 14, 2026 nchini India.
Kifukwe amefariki jana saa 3 usiku kwa muda wa Tanzania, akiwa nchini humo ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Miaka ya 2000, Kifukwe aliwahi kuwa Rais wa klabu ya Yanga ambayo baadaye akawa mjumbe wa baraza lake la wadhamini.
Miongoni mwa mambo ambayo Kifukwe anakumbukwa nayo ni usajili wa wachezaji Saimon Msuva na Jerry Tegete ambao walikuja kuwa mastaa wakubwa wa Yanga.