Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fountain Gate, Polisi Tanzania zarudi nyumbani

NYUMBANI Pict

Muktasari:

  • Fountain Gate ilihamia Arusha, Februari mwaka huu baada ya ombi la Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla na sasa inarudi tena Babati jambo ambalo limethibitishwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

BAADA ya kutumia viwanja vya Black Rhino na Sheikh Amri Abeid vya Arusha kwa miezi minane, timu ya Fountain Gate juzi, Oktoba 16, 2026 ilitangaza rasmi kurejea mkoani Manyara katika mji wa Babati, huku Polisi Tanzania nayo ikirudi nyumbani kwake mkoa wa Kilimanjaro.

Fountain Gate ilihamia Arusha, Februari mwaka huu baada ya ombi la Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla na sasa inarudi tena Babati jambo ambalo limethibitishwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

"Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) inapenda kuutaarifu umma, wadau wa soka na mashabiki wa mpira wa miguu kuhusu mabadiliko ya viwanja vya nyumbani kwa baadhi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC na Ligi ya Championship  kwa msimu wa 2026/2027.

NYUMB 01

Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo: Fountain Gate FC, inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC, itatumia Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara, kama uwanja wake wa nyumbani," ilifafanua taarifa ya TPLB.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mbuni FC na IAA SC, zinazoshiriki Ligi ya Championship ya NBC, zitacheza michezo yao ya nyumbani katika Uwanja wa Agakhan, Arusha.

Wakati Fountain Gate ikirudi Babati, timu ya Polisi Tanzania nayo imeacha kutumia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na sasa itautumia Uwanja wake wa Ushirika uliopo Moshi.

"Aidha, timu ya Polisi Tanzania inarejea kutumia Uwanja wa Ushirika, Kilimanjaro, kama uwanja wake wa nyumbani kufuatia kukamilika kwa maboresho ya uwanja huo, hatua inayowezesha timu hiyo kuendelea kutumia uwanja wake baada ya miundombinu ya uwanja huo kuboreshwa.

NYUMB 02

"Bodi inaendelea kusimamia matumizi bora ya viwanja vya michezo nchini kwa kuzingatia ubora wa miundombinu na kuhakikisha kunakuwepo mazingira mazuri kwa timu, mashabiki na wadau wote wa soka.

"Bodi inawakumbusha wadau na mashabiki wa soka katika mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro kuendelea kujitokeza kwa wingi viwanjani kushuhudia na kuzipa hamasa timu zao zinapocheza michezo ya ligi. TPLB inaamini Ushiriki wao Unaimarisha maendeleo ya soka na kuongeza hamasa ya ushindani katika ligi zetu," imeongeza taarifa hiyo ya Bodi ya Ligi.